Social Icons

Pages

Featured Posts

Monday, January 30, 2017

GOLIKIPA DAVID BURHANI AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa Golikipa wa kutegemewa wa timu za Majimaji ya Songea,Prison na Mbeya City za Jijini Mbeya na hatimaye timu ya Kagera Sugar DAVID ABDALLAH BURHAN amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa kocha wa timu ya Kagera Sugar Meck Mexime, Burhani ameugua tumbo siku tatu zilizopita walipofika Kagera alilazwa kwenye hospitali ya Kiwandani na kuwa baadaye macho yake yalianza kubadilika na kuwa ya njano.
''Tulifanya booking ya ndege kuelekea Bugando, tulichelewa, tukapata jana amefikishwa Bugando leo asubuhi tumepata taarifa kuwa amefariki dunia'' anafahamisha Kocha Mexime.
Hata hivyo anasema kuwa hadi sasa wapo katika taharuki wachezaji wote wanalia, watajaribu kuomba shirikisho la soka liahirishe mechi zake za karibuni hadi hapo watakapomaliza mazishi ya mchezaji mwenzao.
Nimemfahamu David Burhan akiwa timu ya Prison wakati ule akiwa chini ya kocha Juma Mwambusi, baadaye Mwambusi alipohamia Mbeya City naye David Burhani akahamia timu hiyo nadhani kutokana na kocha huyo kutambua umuhimu wa golikipa huyo kwa timu yake mpya.
Chini ya golikipa David Burhan timu hiyo ilifanikiwa kufanya vyema katika ligi hiyo mwaka 2013-14 kiasi cha kushika nafasi ya nne katika ligi hiyo.
Burhani aliondoka katika timu ya Mbeya City na kujiunga na timu ya Kagera Suger hadi kifo kilipomchukua.
Inna Lillahi Waina Ilayhi Rajiuwna!!!!

Saturday, December 31, 2016

NJAA YAPIGA HODI NAMTUMBO MKOANI RUVUMA

Mkulima Omari Mangoto wa kijiji cha Likonde Namtumbo akiwa katika shamba lake lililoathiriwa kwa jua kwa kukosa mvua kwa muda wa wiki tatu
Shamba la Mahindi lililonyauka kwa kukosa mvua Migelegele Namtumbo mkoani Ruvuma
Mche wa mahindi uliokauka kwa kukosa mvua eneo la Likonde Namtumbo mkoani Ruvuma
Mche wa Mahindi uliokauka kwa jua kkwa kukosa mvua eneo la Migelegele Namtumbo mkoani Ruvuma

Mkoa wa Ruvuma ni moja kati ya mikoa sita inayozalisha chakula kwa wingi nchini pamoja na mikoa ya Rukwa,Mbeya,Njombe,Katavi na Iringa, hata hivyo tishio la kuchelewa kunyesha mvua kwa takribani mwezi mmoja limeanza kuwajengea hofu baadhi ya wakazi wa mkoa wa Ruvuma.
Hofu ya kukumbwa na njaa katika msimu wa mavuno wa 2017 imetanda katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kutokana na jua kali linalowaka kukausha mazao yaliyopandwa ambayo yalitegemea mvua iliyotarajiwa kuanza kunyesha mwezi Novemba na Disemba msimu wa kilimo wa 2016-17.
‘’Kipindi hiki ndicho ambacho mvua hunyesha na kurutubisha mazao yaliyopo mashambani, mwaka huu mvua imegoma kabisa mazao yanakauka shambani, kuna dalili kubwa ya njaa msimu huu,’’alisema mkulima mmoja mkazi wa Namtumbo anayelima eneo yalipokuwa mashamba ya NAFCO aliyejitambulisha kwa jina la Kassim Said.
Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka mingine wakati huu mahindi yangekuwa yamefikia urefu wa kima cha futi 4’ hadi futi 5’ na baadhi ya maeneo yangekuwa yameanza kuchanua lakini kutokana na tatizo la mvua hadi sasa mahindi yaliyoanza kuota yamekauka.
Alisema kuwa kwa mbegu za mahindi za muda  mfupi zinatumia muda wa siku 60 ambapo kwa mvua inayonyesha kuanzia mwezi Novemba sasa hivi mahindi yangekuwa yameanza kuchanua bali kwa mbegu ya kawaida inayotumia siku 90 sawa na miezi mitatu kwa sasa ingekuwa imefikia urefu wa futi 5’.
Kwa upande wake mkulima Ayubu Makuti(50) mkulima wa kijiji cha Migelegele wilaya ya Namtumbo alisema kuwa kuna dalili ya njaa mwaka huu kwa kukosa mvua kwa kuwa yeye alianza kupanda mvua za kwanza zilipoanza kunyesha lakini hadi sasa mahindi hayajafika hata urefu wa futi 1’ hali ambayo inaashiria madhara katika msimu huu wa kilimo.
‘’Tuliambiwa kuwa mvua za kwanza ni za kupandia, watu wamepanda mazao yao mapema, mvua imegoma kunyesha kinachofuatia baada ya hapa ni njaa, ukifika shambani wakati wa jua kali mahindi unayaona yakiwa yamenyauka kwa jua,’’alisema Makuti.
Naye mzee Abedi Parahane(80) mkulima wa kijiji cha Migelegele alisema kuchelewa kwa mvua kuna madhara makubwa kwa wakulima wa mazao ya mahindi, mpunga na tumbaku na iwapo haitanyesha hadi ifikapo Januari 10 mwakani wakulima wa Namtumbo watakumbwa na njaa.
‘’Tulijitahidi kuwahi kulima kama desturi yetu, tofauti na mwaka jana watu waliwahi kulima na mvua ilinyesha kwa wakati, unyeshaji wa mvua wa aina hii ni dalili ya njaa’’ alisema Mzee Ali Kilosa(78) mkazi wa kijiji cha Rwinga.
Akizungumza hivi karibuni katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge, Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Luckiness Amlima aliwataka wananchi kutouza chakula chote walichovuna msimu uliopita kutokana na kukosekana kwa mvua ya kutosha msimu huu.
Alisema kukosekana kwa mvua ya kutosha kunaweza kusababisha kuibuka kwa njaa hivyo ili kuepuka fedheha hii ya baa la njaa wananchi wanapaswa kutokuwa na tamaa ya kuuza chakula chote ili kiwasaidie iwapo mvua itaendelea kunyesha kwa kusuasua.
Baadhi ya maeneo ambayo wananchi wamekuwa wakitoa malalalamiko ya mazao yao kukauka na jua ni pamoja na Masuguru, Mtonya, Luegu, Litola, Lusewa,Rwinga, Mandepwende,Likuyu,Mputa na Namtumbo ambako ndiko kunakotegemewa kwa ajili ya mazao ya chakula na biashara kama vile Mahindi, Mpunga,Tumbaku, Mbaazi na Ufuta.

e wa Mahindi uliokauka kwa jua kkwa kukosa mvua eneo la Migelegele Namtumbo mkoani Ruvuma

Thursday, September 8, 2016

*SERIKALI YAJIBU HOJA ZILIZOTOLEWA NA WABUNGE KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA UPATIKANAJI WA TAARIFA*

#Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa utasaidia kuongeza uwajibikaji katika kutoa taarifa juu ya miradi ya maendeleo katika eneo husika.
#Sheria hii itaondoa urasimu wa utoaji wa taarifa katika ofisi za umma.
# Muswada huu unakidhi matakwa ya Katiba ya haki na wajibu kwa wananchi kupata taarifa.
#Muswada huu haukusudii kuficha taarifa zinazohitajika na mtafuta taarifa.
# Muswada huu utasaidia kuwa na utaratibu maalumu wa wananchi kupata taarifa.
# Muswada huu hauzuii haki ya mwananchi yeyote kupata taarifa kwa njia tofauti.
#Muswada huu unaongeza wigo kwa *waandishi wa habari* kwani nao wanahaki ya kupata taarifa.
#Muswada huu unalenga kupanua wigo wa upatikanaji taarifa ili kutekeleza matakwa ya Katiba.
*Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO*
*Dodoma*

Friday, September 2, 2016

KUPATWA KWA JUA KWAVUTIA MAELFU WILAYANI MBARALI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni Kanali Chiku Gallawa wakiangalia Kupatwa kwa Jua eneo la Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya leo asubuhi Jua limepatwa leo kuanzia saa 4:15 hadi saa 7:00 mchana.
Mkazi wa Rujewa akiangalia kupatwa kwa jua kwa kutumia mashine ya kuchomolewa vyuma'Welding' wakati wa kupatwa kwa jua leo mchana.

Raia wa kigeni kutoka nchi za Ujerumani, Uingereza na Sweden wakitumia chombo maalumu cha kuchuja mionzi ya Jua kwa ajili ya kuangalia kupatwa kwa jua katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

Hivi ndivyo kupatwa kwa jua kulivyokuwa kukionekana kwa kupitia chujio maalum la kuchuja mionzi ya jua.

Mkazi wa mjini Rujewa akiangalia kupatwa kwa jua kupitia miwani ya kuchujia mionzi ya jua leo asubuhi.

Mkuu wa wilaya ya Mbarali Reuben Mfune akizungumza wakati wa kupatwa kwa jua mjini Rujewa wilayani Mbarali.

Mbunge wa Mbarali Haroun Pirmohamed akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) Christopher Nyenyembe

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wakishuhudia kupatwa kwa jua leo a

Monday, June 20, 2016

MAKALLA AWAPA SOMO LA KILIMO NA UFUGAJI WATAFITI WA UYOLE

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa somo kwa taasisi za utafiti wa kilimo, mifugo wa chuo cha kilimo Uyole akiwataka kuwekeza zaidi kwenye  utafiti ili kutoa wataalaam bora wa kilimo na ufugaji.
Makalla amesema ili kujitosheleza kwa chakula na mazao ya mifugo nchini wataalamu bora wa utafiti wanahitajika ikiwa ni pamoja na kuwa na malighafi ya Viwanda.
Amesema Rais Dkt John Pombe Magufuli anataka nchi iwe na viwanda vidogo, viwanda vya Kati na vikubwa na kwamba viwanda hivyo vitategemea zaidi malighafi za ndani ambazo zitatokana na kilimo cha kitaalamu sanjari na upatikanaji wa pembejeo bora za kilimo.
Amefafanua kuwa nchi yoyote inayowekeza kwenye utafiti huondokana na matatizo ya kukosekana kwa mbegu bora za mazao ya kilimo na mifugo na hivyo jambo pekee la taasisi za Uyole kutumia teknolojia ya kisasa kwa usindikaji wa mazao ili kuyaongezea thamani.

Kadhalika Makalla amewataka maofisa kilimo,vikundi vya wakulima na wafugaji kutembelea chuo cha Utafiti Uyole ili kujifunza mambo mbalimbali ya kilimo na ufugaji ili kuzalisha kwa tija.