Pages

Monday, March 2, 2015

SAFARI LAGER NYAMA CHOMA YAFIKA KILELE MBEYA, TUMAIN BAR& LODGE WAIBUKA KIDEDEA.

 Mgeni rasmi katika mashindano ya safari lager nyama choma, Katibu tawala wa Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela, akizungumza na wakazi wa Jiji la Mbeya kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
 Meneja wa Bia ya Safari lager Edith Bebwa, akitoa neno la utangulizi kabla ya kuanza kukabidhi zawadi katika fainali ya nyama choma.

 Jaji Mkuu akitaja majina ya washindi
 Mgeni rasmi pamoja na watumishi wa TBL wakijiandaa kuanza kutoa zawadi.
 Mwakilishi wa mshindi wa kwanza ambaye ni Tumain Bar akionesha kombe juu
 Picha ya pamoja washindi wote pamoja na uongozi.
 Meneja wa bia ya safari pamoja na mkuu wa matukio Kanda wakifuatilia kwa makini mashindano ya kuchoma nyama.
 Watumishi wa TBL wakila nyama kwenye moja ya mabanda ya mashindano







 Wateja mbali mbali wakiwa wanapata huduma kwenye mabanda.

BAA ya Tumain iliyopo Ilomba jijini Mbeya imeibuka kinara wa kuchoma nyama katika Fainali iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Chuo cha Uhasibu Mbeya(TIA).
Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari yaliyojulikana kwa jina la Safari lager nyama choma 2015 yalishirikisha baa zaidi ya 20 ambapo baa tano zilitinga fainali.
Mshindi wa kwanza katika fainali hizo Baa ya Tumaini ilijinyakulia Kombe kubwa,Fedha taslimu shilingi Milioni Moja pamoja na Cheti maalumu.
Jaji Mkuu wa Mashindano hayo, Manase alisema mshindi amepatikana kutokana na vigezo ambavyo waliambiwa kwenye semina elekezi kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na usafi wa mazingira yanayochomewa nyama, usafi wa mchomaji mwenyewe,aina ya nyama anayopaswa kuchoma, mazingira kwa ujumla pamoja na utoaji huduma kwa wateja.
Aliitaja baa iliyoibuka msindi wa pili kuwa ni City Pub iliyopo Mwanjelwa iliyojipatia Cheti na fedha shiliki Laki nane, mshindi wa tatu Kalembo baa ya Sokomatola iliyojipatia cheti na shilingi laki sita, msindi wa nne  ni Samaki samaki aliyoibuka na Cheti pamoja na shilingi laki nne huku nafasi ya tano ikienda kwa Nebana  baa iliyopata Cheti na shilingi laki mbili.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika fainali hizo, Quip Mbeyela Katibu tawala Wilaya ya Mbeya, aliipongeza Kampuni  ya Bia TBL kuwa imekuwa ikijitahidi kushirikiana na serikali katika kutoa huduma na kuwawezesha wajasiliamali wadogo.
Aliongeza kuwa  pia Kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kulipa Kodi ambayo imekuwa ikiisaidia Serikali katika kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma kwa jamii.
Naye Meneja wa Bia Safari lager nchini, Edith Bebwa alisema fainali hizo zimeanzia mkoani Mbeya kutokana na wakazi wa Mkoa huo kuongoza katika Unywaji wa bia ya Safari.
Alisema baada ya hapo zoezi hilo litahamia katika mikoa mingine na kuongeza kuwa lengo la mashindano ni kuwawezesha walaji wa nyama wanapata kitu ambacho kimeandaliwa katika mazingira sahihi.
Kwa hisani ya Mbeya yetu Blog

0 comments: