Pages

Saturday, October 3, 2015

MKUTANO WA WADAU WA HABARI NA WANAHABARI KUJADILI MUSTAKABALI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Mkuu wa Kanda Sekretarieti ya Maadili ya Uongozi wa Umma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Erick Mbembati akizungumza na wanahabari katika kikao cha wadau wa habari kwenye ukumbi wa hoteli ya Mbeya Peak.

Kiongozi mwakilishi wa walemavu wa ngozi William Simwali akichangia katika kikao cha wadau wa habari.
Mwandishi wa habari Mwandamizi Laauden Mwambona akichangia mada katika kikao cha wadau na wanahabari.

Mwandishi wa habari na mpigapicha mkongwe Jonas Mwasumbi akichangia hoja kwenye mjadala wa kikao cha wadau wa habari na wadau kwenye ukumbi wa Hotel ya Mbeya Peak.

Mwandishi wa habari Festo Sikagonamo akisisitiza jambo kwenye kikao cha wadau na wanahabari mchana huu kwenye ukumbi wa Mbeyaa Peak Hotel




WANAHABARI na waandishi wa habari wametakiwa kujiamini na kujitathmini weledi wao katika utendaji wao wa kazi za kihabari ili kujiwekea mazingira salama wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 25,2015.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kanda Sekretarieti ya Maadili ya Viomngozi wa Umma kanda ya Nyanda za Juu kusini Erick Mbembati katika kikao kilichohusisha wadau wa habari na waandishi kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mbeya Peak Jijini Mbeya mchana huu.

Mbembati alisema kuwa waandishi kama wanataaluma wengine wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ili kuiepusha nchi kuingia katika majanga ambayo yangeweza kuepukika.

Alisema pamoja na wanahabari kutakiwa kufanya kazi kwa maadili pia wamiliki wa wa vyombo ambavyo wanahabari hao wanavitumikia wanatakiwa kuthamini mchango wao ikiwa ni pamoja na kuwajali na kuiwapa stahiki zao kwa wakati.

''Waandishi wengi hawana mkataba wanafanya kazi katika wakati mgumu, wamiliki wao hawathamini mchango wao, hili linasababisha waingie katika mgogoro na hata kutumiwa na watu wasiokuwa wema kwa kuwapa rushwa'', alisema.

Mbembati alisema kuwa wino wa wanahabari unaweza kusababisha kuibuka kwa vita na umwagikaji wa damu hivyo ni vyema wakawa na tahadhari kubwa wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 25.

Aidha alisema wanahabari wanatakiwa kufanya kazi kwa kujituma ikiwa ni pamoja na kujiheshimu na kuheshimiana katika kazi zao na kwamba hili litachangia heshima kwa wanahabari na kuheshimiwa.

0 comments: