Pages

Tuesday, May 31, 2016

MELI TATU ZENYE THAMANI YA BILIONI 24 ZAJENGWA KUHUDUMIA ZIWA NYASA



Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) wakipewa maelekezo juu ya ujenzi wa cherezo cha kutengenezea Meli kwenye Bandari ya Itungi Ziwa Nyasa wilayani Kyela
 




Meli ya Mizigo inayotarajia kubeba tani 200 iliyokamilika kwa asilimia 95 inayotarajia kuanza kazi mwezi Agosti mwaka huu

Cherezo kinachotumika kujengea Meli na kutengeneza Meli zilizoharibika kikiwa katika Bandari ya Itungi Ziwa Nyasa


Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro Marine, Saleh Songoro akiwa na waandishi wa habari za Utalii an Uwekezaji Tanzania(TAJATI) ambao walitembelea kuangalia ujenzi wa meli tatu zinazojengwa bandarini hapo

Mkondo wa mto Mbasi unaoungana na Ziwa Nyasa kwenye Bandari ya Itungi wilayani Kyela




Meli ya MV Songea iliyotia nanga Bandari ya Kiwira miezi miwili iliyopita bado iko bandarini hapo haijang'oa nanga


Zaidi ya Sh24 bilioni zinatarajia kutumika katika miradi mitatu ya kuunda  meli   na chelezo kwenye  bandari ya Itungi  katika  Ziwa  Nyasa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.
Akizungumza na Waandishi wa  Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (Tajati)Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya Songoro Marine,Salehe Songoro alisema kuwa mradi wa kwanza ni wa kusafirisha wa chelezo kutoka jijini Mwana na kuunda upya katika bandari ya Itungi.
Alisema mradi huo wa kusafirisha chelezo na kuunda upya umegharimu Sh2.99bilioni  kazi ambayo imekamilika kwa asilimia 95 huku meli ya abiria yenye uwezo wa kubeba tani 200, abiria 200 magari  madogo 12 yakiwemo mabasi matatu ya abiria imeshaanza kutengenezwa.
Songoro alisema mradi wa pili ni wa kutengeneza meli moja ya abilia na mizigo  ambayo ujenzi wake tayari umeshaanza na hadi sasa umefikia  asilimia 30   na kwamba hadi kukamilika utagharimu  kiasi cha Sh 10.35 bilioni.
Alisema kuwa mradi wa tatu ni wa uundwaji  wa meli mbili za mizigo ambao utagharimu kiasi cha Sh11.253bilioni ambao  umefikia asilimia 75 ambapo uwezo wa meli hizo mbili za mizigo ni tani 1566.166.
Kwa upande wake  Mkuu wa  Bandari   ya Itungi Percival  Salama alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kukuza uchumi kwa Wilaya ya Kyela na kwamba kutatoa fursa kwa wananchi kupata urahisi wa kusafiri kwani kwa sasa katika badari hiyo hakuna meli.
“Uwekezaji unaofanywa katika badari hii utakuwa na manufaa kuanzia sasa hadi mika ya baadae kwani masoko yapo lakini tatizo ni ukosefu wa meli ya uhakika na pia itakuwa ni kivutio kikubwa cha utalii kwani kila mmoja atapenda kufika katika badari hiyo na kusafiri na meli ambayo itakuwa ya kisasa.’alisema.
Alisema awali uundaji na ukarabati wa meli kwa ajili ya ziwa hilo huwa unafanyika nchini Malawi ambapo hadi sasa kuna meli moja inayoitwa MV Songea ambayo inamiezi miwili tangu imefika  katika  bandari ya Kiwira.

0 comments: