Featured Posts
Wednesday, March 8, 2017
Monday, February 27, 2017
Monday, January 30, 2017
GOLIKIPA DAVID BURHANI AFARIKI DUNIA
Aliyewahi kuwa Golikipa wa kutegemewa wa timu za Majimaji ya
Songea,Prison na Mbeya City za Jijini Mbeya na hatimaye timu ya Kagera
Sugar DAVID ABDALLAH BURHAN amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali
ya Bugando jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa kocha wa timu ya Kagera
Sugar Meck Mexime, Burhani ameugua tumbo siku tatu zilizopita walipofika
Kagera alilazwa kwenye hospitali ya Kiwandani na kuwa baadaye macho
yake yalianza kubadilika na kuwa ya njano.
''Tulifanya booking ya
ndege kuelekea Bugando, tulichelewa, tukapata jana amefikishwa Bugando
leo asubuhi tumepata taarifa kuwa amefariki dunia'' anafahamisha Kocha
Mexime.
Hata hivyo anasema kuwa hadi sasa wapo katika taharuki
wachezaji wote wanalia, watajaribu kuomba shirikisho la soka liahirishe
mechi zake za karibuni hadi hapo watakapomaliza mazishi ya mchezaji
mwenzao.
Nimemfahamu David Burhan akiwa timu ya Prison wakati ule
akiwa chini ya kocha Juma Mwambusi, baadaye Mwambusi alipohamia Mbeya
City naye David Burhani akahamia timu hiyo nadhani kutokana na kocha
huyo kutambua umuhimu wa golikipa huyo kwa timu yake mpya.
Chini
ya golikipa David Burhan timu hiyo ilifanikiwa kufanya vyema katika ligi
hiyo mwaka 2013-14 kiasi cha kushika nafasi ya nne katika ligi hiyo.
Burhani aliondoka katika timu ya Mbeya City na kujiunga na timu ya Kagera Suger hadi kifo kilipomchukua.
Inna Lillahi Waina Ilayhi Rajiuwna!!!!
Saturday, December 31, 2016
NJAA YAPIGA HODI NAMTUMBO MKOANI RUVUMA
Mkulima Omari Mangoto wa kijiji cha Likonde Namtumbo akiwa katika shamba lake lililoathiriwa kwa jua kwa kukosa mvua kwa muda wa wiki tatu |
Shamba la Mahindi lililonyauka kwa kukosa mvua Migelegele Namtumbo mkoani Ruvuma |
Mkoa wa Ruvuma ni moja kati ya mikoa sita inayozalisha chakula kwa wingi nchini pamoja na mikoa ya Rukwa,Mbeya,Njombe,Katavi na Iringa, hata hivyo tishio la kuchelewa kunyesha mvua kwa takribani mwezi mmoja limeanza kuwajengea hofu baadhi ya wakazi wa mkoa wa Ruvuma.
Hofu ya
kukumbwa na njaa katika msimu wa mavuno wa 2017 imetanda katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kutokana na jua kali linalowaka kukausha mazao yaliyopandwa
ambayo yalitegemea mvua iliyotarajiwa kuanza kunyesha mwezi Novemba na Disemba
msimu wa kilimo wa 2016-17.
‘’Kipindi
hiki ndicho ambacho mvua hunyesha na kurutubisha mazao yaliyopo mashambani,
mwaka huu mvua imegoma kabisa mazao yanakauka shambani, kuna dalili kubwa ya
njaa msimu huu,’’alisema mkulima mmoja mkazi wa Namtumbo anayelima eneo
yalipokuwa mashamba ya NAFCO aliyejitambulisha kwa jina la Kassim Said.
Alisema kuwa
kwa kipindi cha miaka mingine wakati huu mahindi yangekuwa yamefikia urefu wa
kima cha futi 4’ hadi futi 5’ na baadhi ya maeneo yangekuwa yameanza kuchanua
lakini kutokana na tatizo la mvua hadi sasa mahindi yaliyoanza kuota yamekauka.
Alisema kuwa
kwa mbegu za mahindi za muda mfupi
zinatumia muda wa siku 60 ambapo kwa mvua inayonyesha kuanzia mwezi Novemba
sasa hivi mahindi yangekuwa yameanza kuchanua bali kwa mbegu ya kawaida
inayotumia siku 90 sawa na miezi mitatu kwa sasa ingekuwa imefikia urefu wa
futi 5’.
Kwa upande
wake mkulima Ayubu Makuti(50) mkulima wa kijiji cha Migelegele wilaya ya
Namtumbo alisema kuwa kuna dalili ya njaa mwaka huu kwa kukosa mvua kwa kuwa
yeye alianza kupanda mvua za kwanza zilipoanza kunyesha lakini hadi sasa
mahindi hayajafika hata urefu wa futi 1’ hali ambayo inaashiria madhara katika
msimu huu wa kilimo.
‘’Tuliambiwa
kuwa mvua za kwanza ni za kupandia, watu wamepanda mazao yao mapema, mvua
imegoma kunyesha kinachofuatia baada ya hapa ni njaa, ukifika shambani wakati
wa jua kali mahindi unayaona yakiwa yamenyauka kwa jua,’’alisema Makuti.
Naye mzee
Abedi Parahane(80) mkulima wa kijiji cha Migelegele alisema kuchelewa kwa mvua
kuna madhara makubwa kwa wakulima wa mazao ya mahindi, mpunga na tumbaku na
iwapo haitanyesha hadi ifikapo Januari 10 mwakani wakulima wa Namtumbo
watakumbwa na njaa.
‘’Tulijitahidi
kuwahi kulima kama desturi yetu, tofauti na mwaka jana watu waliwahi kulima na
mvua ilinyesha kwa wakati, unyeshaji wa mvua wa aina hii ni dalili ya njaa’’
alisema Mzee Ali Kilosa(78) mkazi wa kijiji cha Rwinga.
Akizungumza
hivi karibuni katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma
Dkt.Binilith Mahenge, Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Luckiness Amlima aliwataka
wananchi kutouza chakula chote walichovuna msimu uliopita kutokana na
kukosekana kwa mvua ya kutosha msimu huu.
Alisema
kukosekana kwa mvua ya kutosha kunaweza kusababisha kuibuka kwa njaa hivyo ili
kuepuka fedheha hii ya baa la njaa wananchi wanapaswa kutokuwa na tamaa ya
kuuza chakula chote ili kiwasaidie iwapo mvua itaendelea kunyesha kwa kusuasua.
Baadhi ya
maeneo ambayo wananchi wamekuwa wakitoa malalalamiko ya mazao yao kukauka na
jua ni pamoja na Masuguru, Mtonya, Luegu, Litola, Lusewa,Rwinga,
Mandepwende,Likuyu,Mputa na Namtumbo ambako ndiko kunakotegemewa kwa ajili ya
mazao ya chakula na biashara kama vile Mahindi, Mpunga,Tumbaku, Mbaazi na
Ufuta.
Labels:
habari picha
Thursday, September 8, 2016
*SERIKALI YAJIBU HOJA ZILIZOTOLEWA NA WABUNGE KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA UPATIKANAJI WA TAARIFA*
#Sheria hii itaondoa urasimu wa utoaji wa taarifa katika ofisi za umma.
# Muswada huu unakidhi matakwa ya Katiba ya haki na wajibu kwa wananchi kupata taarifa.
#Muswada huu haukusudii kuficha taarifa zinazohitajika na mtafuta taarifa.
# Muswada huu utasaidia kuwa na utaratibu maalumu wa wananchi kupata taarifa.
# Muswada huu hauzuii haki ya mwananchi yeyote kupata taarifa kwa njia tofauti.
#Muswada huu unaongeza wigo kwa *waandishi wa habari* kwani nao wanahaki ya kupata taarifa.
#Muswada huu unalenga kupanua wigo wa upatikanaji taarifa ili kutekeleza matakwa ya Katiba.
*Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO*
*Dodoma*
Labels:
habari picha
Friday, September 2, 2016
KUPATWA KWA JUA KWAVUTIA MAELFU WILAYANI MBARALI
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni Kanali Chiku Gallawa wakiangalia Kupatwa kwa Jua eneo la Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya leo asubuhi Jua limepatwa leo kuanzia saa 4:15 hadi saa 7:00 mchana. |
Mkazi wa Rujewa akiangalia kupatwa kwa jua kwa kutumia mashine ya kuchomolewa vyuma'Welding' wakati wa kupatwa kwa jua leo mchana. |
Raia wa kigeni kutoka nchi za Ujerumani, Uingereza na Sweden wakitumia chombo maalumu cha kuchuja mionzi ya Jua kwa ajili ya kuangalia kupatwa kwa jua katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya. |
Hivi ndivyo kupatwa kwa jua kulivyokuwa kukionekana kwa kupitia chujio maalum la kuchuja mionzi ya jua. |
Mkazi wa mjini Rujewa akiangalia kupatwa kwa jua kupitia miwani ya kuchujia mionzi ya jua leo asubuhi. |
Mkuu wa wilaya ya Mbarali Reuben Mfune akizungumza wakati wa kupatwa kwa jua mjini Rujewa wilayani Mbarali. |
Mbunge wa Mbarali Haroun Pirmohamed akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) Christopher Nyenyembe |
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wakishuhudia kupatwa kwa jua leo a |
Labels:
habari picha
Monday, June 20, 2016
MAKALLA AWAPA SOMO LA KILIMO NA UFUGAJI WATAFITI WA UYOLE
Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya Amos Makalla ametoa somo kwa taasisi za utafiti wa kilimo, mifugo wa
chuo cha kilimo Uyole akiwataka kuwekeza zaidi kwenye utafiti ili kutoa wataalaam bora wa kilimo na ufugaji.
Makalla
amesema ili kujitosheleza kwa chakula na mazao ya mifugo nchini wataalamu bora wa
utafiti wanahitajika ikiwa ni pamoja na kuwa na malighafi ya Viwanda.
Amesema Rais
Dkt John Pombe Magufuli anataka nchi iwe na viwanda vidogo, viwanda vya Kati na
vikubwa na kwamba viwanda hivyo vitategemea zaidi malighafi za ndani ambazo
zitatokana na kilimo cha kitaalamu sanjari na upatikanaji wa pembejeo bora za
kilimo.
Amefafanua
kuwa nchi yoyote inayowekeza kwenye utafiti huondokana na matatizo ya kukosekana
kwa mbegu bora za mazao ya kilimo na mifugo na hivyo jambo pekee la taasisi za
Uyole kutumia teknolojia ya kisasa kwa usindikaji wa mazao ili kuyaongezea
thamani.
Kadhalika Makalla amewataka maofisa kilimo,vikundi vya wakulima na wafugaji kutembelea chuo cha Utafiti Uyole ili kujifunza mambo mbalimbali ya kilimo na ufugaji ili kuzalisha kwa tija.
Kadhalika Makalla amewataka maofisa kilimo,vikundi vya wakulima na wafugaji kutembelea chuo cha Utafiti Uyole ili kujifunza mambo mbalimbali ya kilimo na ufugaji ili kuzalisha kwa tija.
Labels:
habari picha
Subscribe to:
Posts (Atom)