Mshindi wa kwanza wa Miss Mbeya vijijini aliyekaa akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Pendo Nelson na watatu Neema Tadei
Washiriki wa shindano la uremb la Miss Mbeya vijijini wakitoa burudani mbele ya wageni waalikwa katika ukumbi wa Royal Tughimbe Mbalizi Mbeya vijijini.
Kikundi cha burudani kutoka Mbalizi kikionyesha show kali kama mfano wa kikundi cha THT
Warembo wakionyesha show
Jaji msaidizi wa mashindano ya kumsaka Miss Mbeya vijijini Mary Gumbo akizungumza katika mashindano hayo
.
Mkazi wa kijiji cha Mbalizi Atukuzwe Fabiani jana aliibuka mshindi wa
Miss Mbeyavijijini baada ya kubwaga warembo wenzie 12 katika
mashindano yaliyofanyika katika ukumbi wa Royal Tughimbe na
kujinyakulia zawadi ya seti Kompyuta yenye thamani ya ya Sh 800,000.
Akitangaza matokeo ya mashindano hayo jaji mkuu wa mashindano hayo Maulid Lyoba ambaye ni afisa mauzo wa kampuni ya bia ya TBL alisema kuwa nafasi ya pili imechukuliwa na Pendo Nelson ambaye alizawadiwa meza ya kioo (Dressing table).
Lyoba alimtaja mshindi wa tatu katika mashindano hayo kuwa ni Neema Tadei ambaye alikabidhiwa zawadi ya seti ya radio yenye thamani ya Sh250,000.
Akizungumzia ushindi huo mrembo huyo Miss Mbeyavijijini alisema kuwa atatumia nafasi hiyo katika kuhamasisha jamii kuwasaidia watotoambao wameshindwa kuendelea na shule na wale wa mitaani.
"Nashukuru nimeshinda nafasi hii na ninaahidi sitobweteka nitaitumia vizuri kwa kuhakikisha nashiriki katika shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kuihamasisha serikali kuongeza vitanda katika wodi za wakina mama wajawazito na watoto na wakina mama kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali"alisema
0 comments:
Post a Comment