Pichani ni mgonjwa
Wordson Pakyindi akitembea kwa kutumia magongo mara baada ya kuunganishwa
mifupa kwa kutumia dawa za miti shamba na wanyama baada ya kupata ajali na
kuvunjika mguu ,nyuma yake ni mganga wa asili aliyemtibu Anyimike Mabeja
katika kijiji cha Bwenda Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya.
Pichani ni mganga wa asili
anayeunganisha mifupa kwa kutumia dawa za miti shamba na Wanyama Anyimike
Mabeja akimwangalia mgonjwa wake Wordson Pakyindi sehemu ambayo amemuunganisha
mifupa kwa kutumia dawa hizo katika kijiji cha Bwenda Wilaya hya
Ileje Mkoani Mbeya.
Pichani ni mgonjwa Wordson Pakyindi akitembea kwa kutumia magongo mara baada ya kuunganishwa mifupa kwa kutumia dawa za miti shamba na wanyama baada ya kupata ajali na kuvunjika mguu ,nyuma yake ni mganga wa asili aliyemtibu Anyimike Mabeja katika kijiji cha Bwenda Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya.
Ajali
za barabarani, vipigo kwa kiasi kikubwa vimekuwa vikichangia watu wengi
kupata ulemavu wa kudumu na wengine kulazimika kuondolewa kabisa viungo
vyao kwa kuvikata kutokana na kuonekana kitaalamu havitaweza kutibika
tena.
Tishio
la kupata ulemavu limekuwa likitia hofu watu wengi kutokana na ukweli
kuwa pindi mtu anapopata ulemavu, uwezo wa kufanya shughuli za kiuchumi
unapungua kwa kiasi kikubwa na mtu kuanza kulazimika kwa kiwango fulani
kuwa tegemezi.
Lakini
wakati wananchi wakikabiliwa na changamoto mbalimali za kupata huduma
katika Hospitali nchini, huenda tumaini jipya likawa limepatikana
kutokana na kuibuka kwa mtaalamu wa tiba mbadala ya kuunganisha mifupa
na kutibu majeraha kwa kutumia dawa za miti shamba na wanyama.
Mabeja
ni mtoto wa sita katika familia ya mzee
Patisi Mabeja anasema kuwa alianza kutoa tiba hiyo baada ya kurithi kutoka kwa
baba yake ambaye pia kazi hiyo alirithi kutoka kwa baba yake ambaye alikuwa akitoa
tiba hiyo wakati wa ukoloni kutokana na mazingira waliyokuwa wakiishi kutokuwa
na hospitali na wataalam wa dawa za kisasa kwa ajli ya kutoa tiba hiyo mara
wanapokuwa wamepatwa na matatizo ya kuvunjika mifupa.
“Huu utaalam
ni kutoka kwa mababu zetu alianza kufanya babu yake baba akaja baba yake
baba na baadae akaja baba yangu ambaye
ndiye aliyenirithisha mimi kutokana na hali ya baba kwa sasa hajiwezi anaumri zaidi ya miaka 90”anasema
Anasema kuwa
baba yake mzazi alianza kutoa tiba hiyo mwaka 1982 ambapo watu wengi wa kutoka
vijiji mbali mbali wamekuwa wakipata tiba kutoka kwa huyo baba na wamekuwa
wakipona huku akiwa anajifunza na kwamba baba yake huyo aliweza kumshirikisha
kwa ukaribu na kutoa maelekezo jinsi dawa hiyo inavyotibu na inavyopatikana.
Dawa inayotumika katika kutoa tiba
hiyo
Mabeja
anaeleza aina ya dawa inayotumika katika kutoa tiba hiyo kuwa ni mizizi ,
majani na wanyama ambapo mizizi inaitwa Mlumila
kwa Lugha ya Kindali na upande wa majani dawa hiyo inaitwa Nalutete na
Nakisokoso.
Anasema kuwa
shughuli za kuunganisha mifupa zinaendana tiba ya kansa hivyo na kuwalazimu
kutumia dawa ya ugonjwa wa Kansa pamoja
na dawa hizo katika kutoa tiba ambapo dawa hiyo ya kansa inatokana na Wanyama ambao
ni Kapenka(Panya buku),jamii ya nyani wenye rangi nyeupe(Mbega)na mdudu ambaye
anapenda kukaa kwenye matope(Kabhwa kabhwa).
Mabeja
anaeleza kuwa dawa hizo zinapatikana polini ambapo kuna umbali mrefu una kulazimika
kutumia siku mbili hadi tatu kwenda kurudi nyumbani kwake kutokana na mazingira
ya kijijini yalivyo hivyo ulazimika kutembea kwa mguu kwa siku hizo .
Jinsi anavyofanya kazi ya kutoa tiba
hiyo
“Ninaotaalam
wa kugundua tatizo hata bila kutumia picha kama wanavyofanya hospitalini hivyo
ninauwezo kugundua ni aina gani ya mfupa ambao umevunjika na jinsi ya kupunguza mfupa na kuupanga vizuri” hunichukua
nyumbani
Anasema kuwa
kuna mifupa ambayo inatoka nje na mingine ipo ndani kwa ndani ambapo hutumia utaalam aliofundishwa na babu zake jinsi ya kutambua tatizo na jinsi ya kulitibu na mgonjwa anapona
kwa kutumia dawa ya ganzi ya
hospitalini.
Anafafanua
kuwa mara baada ya wagonjwa kumaliza matibabu kwake huwa anawashauri kwenda hospitali kwa ajili ya
uchunguzi zaidi na kujiridhisha kama amepona “wengi wamefanya hivyo na wamekuwa
wakipona kabisa”anasema
Anasema kuwa
amekuwa akiwapokea wagonjwa ambao
wameshindwa kupata tiba kutoka kwenye hospitali mbali mbali ikiwa ni pamoja na
rufaa Mbeya ambao wanakuwa na taarifa ya
uwepo wake na wengine humchukua nyumbani kwake na kwenda
kutoa tiba kwa wagonjwa ambao wana hali mbaya na hawana uwezo wa kutembea.
Mganga huyo
anasema kuwa enzi za mababu mawahgonjwa walikuwa wanatoa mbuzi mmoja kama
gharama ya matibabu lakini kwa sasa wanatoa shilingi 70,000 pekee ambayo ndiyo
gharama ya mbuzi mmoja kwa wakati huu.
Anasema kuwa
amekuwa akipata ushirikiano kutoka kwa serikali ya kijiji,kata na hospitali
teule ya Wilaya ya Ileje ia Isoko ambapo humsaidia kupata vifaa vya kuvaa
mkononi(Gloves) wakati wa kutoa tiba na dawa ya ganzi .
Changamoto anazokumbana nazo katika
kutoa tiba hiyo
Mabeja anaeleza changamoto anazokutana nazo ikiwa ni
pamoja ukosefu wa usafiri kwa ajili ya kwenda kutafuta dawa,ukosefu wa
mawasiliano hapo kijijini kwake na hivyo kushindwa kuwasiliana na wagonjwa wake
.
“Huku kwetu
hakuna mawasiliano kama unavyokuona mazingira yake hivyo nashindwa kabisa
kuwasiliana na wagonjwa wangu kwani nimeweza kuwahudumia wagonjwa kutoka ndani
ya mkoa na nje kama vile Mkoa wa Morogoro na iringa ambako nimekwenda kutoa
huduma na huwa na tibu wagonjwa 20 kwa mwezi”anasema
Kauli ya mgonjwa aliyepata tiba hiyo
Mkazi wa
kijiji cha Kyimo Wilaya ya Rungwe Wordson
Pakyindi(30)ni mgonjwa ambaye amepatiwa tiba na mganga huyo mara baada ya
kupata ajali ya pikipiki na kuvunjika mguu naeleza jinsi alivyopata tiba kutoka
kwa mganga huyo.
Anasema kuwa
alipata ajali ya pikipiki baada ya kugongwa na gari aiana ya Toyota Hiace
Desemba 17,2013 katika eneo la Igawilo uyole
jijini Mbeya akiwa anakwenda kazini kusababisha kuvunjika mguu wa kushoto na
paja kupasuka na kusababisha kuwepo kwa kidonda kikubwa ikiwa ni pamoja na goti
kuhama katika sehemu yake.
“Baada ya
ajali hiyo wasamalia wema walinibena ma kunipeleka katika hospitali ya rufaa
mbeya ambpo nilipatiwa huduma ya kwanza kwa nishona sehe,u ya paja iliyokuwa na
kidonda na wakati napelekwa kwenye chumba cha kupigwa picha (x-ray)nilifuatwa
muuguzi aliyekuwa ananihudumia na kuniambia kuwa wenzio wanokuja hapa huwa
wanatoa fedha ndipo wanahudumiwa vizuri kauli hiyo iliniongezea maumivu”anasema
Anasema kuwa
baada ya kupiga picha hiyo alipelekwa wodini
ambapo madaktari walimwambia kuwa anatakiwa
kuwekwa chuma bila ganzi kutokana shinikizo la damu kuwa chini (BP Kushuka)”hali
ambayo nilikataa kuwa siwezi kuwekwa chuma bila kutokana na maumivu makali
niliyokuwa nayapata wakati ule”anasema
“Niliwaeleza
ndugu zangu kuwa sipo tayari kuwekwa chuma bila ganzi na ndipo alipokuja kaka
yangu na kuniambia kuwa huku kuna mganga ambaye angeweza kunitibu na nikapona
hivyo nilimkubalia kuja huku kwani nili kuwa siwezi kuinuka,kukaa wala kugeuka
zaidi ya kulala pekee”anasema
Anasema kuwa
waliondoka hospitalini hapo kwa kuwaeleza wauguzi kuwa wameamua kwenda
hospitali ya mission Peramiho Mkoa Ruvuma na kufanikiwa kuruhusiwa kuondoka hospitalini
hapo siku ya pili mara baada ya ajali.
“Nilipokuwa
natoka rufaa hali yangu ilikuwa mbaya
kwani huduma niliyokuwa nimepa ni ya kushonwa kidonda ili kisiendelee kutoka damu nilikuwa siwezi
kutembea wala kutikisika nilikuwa nabebwa kama jiwe lakini namshukuru mungu
mara baada ya kufika hapa hali yangu ni nzuri kwa sasa naweza hata kuinuka peke
yangu na kuchukua magongo yangu na kuanza kutoka nje”anasema
Anasema kuwa
mara baada ya kufika hapo mganga huyo aliweza kuunganisha mfupa bila ya kuwekwa chuma na goti
kulirudisha sehemu yake na kwamba kkwa sasa kidonda kimepona kilichobaki ni
goti ambalo limesababisha atumie msaada wa magongo katika kutembea.
“Namshukuru
sana huyu mganga kwani ameokoa maisha yangu kwani ningeweza kupata ulemabu wa
maisha lakini amenitibu vizuri na nimeridhika kama unavyoniona hapa na muda
siyo mrefu nitarudi nyumbani na
kuendelea na kazi zangu najiona nimepona ni hili goti ndiyo bado kidogo kupona “anasema
Mgonjwa huyo
ameiomba serikali kuwa karibu na mganga
huyo ili kuweza kumuwezesha katika kutoa tiba yake na kuweza kuwasaidia
wagonjwa hasa wale ambao wanakuwa hawana uwezo wa kumudu gharama kubwa ambazo
zimekuwa zikitozwa katika hospitali kubwa zenye uwezo wa kutibu magonjwa kama
hayo.
“Serikali
isiangalie waganga wale wanaojitangaza kwa mabango makubwa na kwenye vyombo vya habari mganga wa ukweli hajitangazi bali anafuatwa
hivyo ni vema wakamtumia huyu mganga kwa ajili ya kuokoa nguvu kazi kubwa ambayo imekuwa ikipotea kutokana na
baadhi ya watu kuwa na ulemavu wa maisha kwa kukatwa miguu”anasema
Naye
Abduwnuwasi Kalinga mkazi wa kijiji cha Bwenda anasema kuwa mganga huyo amekuwa
ni msaada mkubwa katika eneo hilo watu wengi wamekuwa wakipata ajali katika
shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kucheza mpira na kuanguka kwenye mti.
“Tumeshuhudia
watu wengi ambao wamefika kwa mganga huyu na wamepona na kwa hapa kwetu
kijijini vijana wengi wamehudumiwa na huyu mganga na wamepona bila hata ya
kwenda hospitali kama unavyojua kutoka hapa kwenda hospitalini ni mbali sana na usafiri hakuna hivyo wote
tunamtegemea huyu mganga kwa ajili ya kupata tiba hapa”anasema
anasema kuwa
tatizo siyo serikali bali ni watoa huduma katika hospitali kuwaona wagonjwa kwa
kutanguliza masilahi yao binafsi badala ya kutoa huduma kwanza na hivyo
kusababisha watu masikini kupata ulemavu wakudumu kutokana na kushindwa kumudu
gharama za matibabu.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa halmshauri ya Wilaya ya Ileje Sylivia Siliwa anasema kuwa
mganga huyo wanamfahamu na wagonjwa wengi wamepona kupitia tiba yake ila bado
hajajisajili na kuweza kutambulika kama
waganga wengine wa tiba ya asili.
“Nimemsikia
na halmshauri yetu inafahamu kuwepo kwa mganga huyu lakini bado hajajisajili
kwani anatakiwa kujisajili na kujiunga na umoja wa waganga wa tiba ya asili ili
aweze kupata kibali na kuweza kutambulika kisheria”anasema
Anasema kuwa
kinachotakiwa kwa sasa ni mganga huyo kuanza utaratibu wa kuhakikisha anajiunga
na umoja huo ambao utamsaidia kutambulika kishera na kuweza kupata msaada wa
aina yoyote ambao anauhitaji kutoka halmashauri
na kuweza kutoa tiba yake vizuri na kwa
watu wengi.
0 comments:
Post a Comment