Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akionyesha Bunduki aiana ya ShortGun iliyokamatwa kwenye tukio la majibizano ya risasi baina ya majambazi na askari polisi katika eneo la Msikitini Mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya na kusababisha kifo cha jambazi mmoja .
Baadhi ya wandishi wa habari Mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye chumba cha mikutano katika ofisi ya kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya
MBEYA.Mtu mmoja anayesadikika kuwa ni jambazi ameuwawa katika tukio la kurushiana risasi na askario polisi na
kupigwa risasi ubavu katika eneo la msikitini mji mdongo wa Tunduma
Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya.
Akizungumza na waandishi habari ofisini kwake kamanda wa
polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi
alisema kuwa tukio hilo lilitokea leo
majira ya saa 11 Alfajili baada ya
marehemu huyo akiwa na mwenzake kurushiana risasi na askari polisi mara baada
ya kujaribu kuwasimamisha.
Alisema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa
Walinzi wa usiku katika eneo hilo kuwatilia shaka watu hao kuwa wanania ya kufanya uhalifu wa kutumia silaha na ndipo
askari waliokuwa doria walifika katika eneo hilo na kufanya msako mkali.
“Kutokana na taarifa hizo msako mkali ulianza wa kuwatafuta watuhumiwa
na ilipofika majira ya saa 11:00 alfajili ya leo walikutana na watu wawili waliowatilia shaka
kutokana na jinsi walivyovaa kulingana
maelekezo yaliyotolewa na walinzi “alisema
Msangi alisema kuwa
kati ya watu hao mmoja alikuwa amevaa
jaketi kubwa jeusi na mwingine akiwa amebeba mfuko mkubwa ,
wakati polisi wakijaribu
kuwasimamisha watu hao walianza kukimbia
na mmoja aliyekuwa amevaa jaketi alipofika umbali wa mita 20 alitoa silaha
bunduki na kuanza kufyatua risasi ovyo uelekero wa askari.
“Baada ya kuona hivyo askari walijibu na katika majibizano
hayo ya kurushiana risasi jamabazi mwenye silaha alipigwa risasi
ubavuni na kufariki dunia papo hapo na
kufanikiwa kukamata bunduki moja aiana
ya AK – 47 yenye namba 592058
ikiwa na risasi 25 kwenye magazine
yenye uwezo wa kubeba risasi 30”alisema
Alisema kuwa
mtuhumiwa mmoja aliyekuwaamaebeba mfuko
mkubwa alifanikiwa kukimbia na
kwamba baada ya upekuzi marehemu
alikutwa na kitambulisho cha mpiga kura chenye jina la Joseph Thadei Kapinga mzaliwa
Songea Ruvuma lakini
ni mkazi wa Mafiga Morogoro.
Alisema kuwa katika tukio
hakuna madhara yoyote yaliyotokewa kwa wanananchi na ashkari polisi na kwamba upelelezi unaendelea ikiwa ni
pamoja na kumtafuta mtuhumiwa aliyerkimbia pamoja na mtandao wao wa ujambazi.
0 comments:
Post a Comment