Mbeya.Watu wawili wamekufa
papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa baada ya
kugongwa na basi la kampuni ya Newforce kuligonga gali lingine aina ya Fuso na kuacha
njia na kuwagonha watembea kwa mguu katika kijiji cha Igurusi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya .
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi
aliwataja waliokufa katika ajali hiyo
kuwa ni pamoja na Theresia Hingi (65) na Mary Kizito (26) wote wakazi wa igurusi ambapo walifariki papo hapo.
Alisema kuwa kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa
12:00 jioni katika kijiji cha Igurusi
barabara ya Mbeya Njombe na kuhusisha
basi la kampuni ya Newforce lenye namba za usajili T. 952 CGU aina ya Scania.
Msangi kuwa basi hilo
lilikuwa likitokea jijini Dar es
salaam kuja Mbeya lilipofika
katika eneo la Igurusi liligonga gari linginel enye namba za usajili T. 954 AMH
aina ya Fuso lililokuwa
likiendeshwa na Tupa Anyosisye(32) mkazi wa Kiwira tukuyu na kasha kuacha njia na kuwagonga watembea
kwa mguu.
Alisema kuwa katika ajali hiyo watu wengine wanne wamejeruhiwa kati yao ni abiria mwanaume mmoja na wanawake
watatu watembea kwa miguu ambao majina
yao hayajafahamika na kwamba walikimbizwa katika hospitali ya mission Chimala.
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni mwendo
kasi wa basi la Newforce na kwamba dereva wa basi hilo alikimbia mara
baada ya ajali na jeshi la polisi
linaendelea kumsaka kwa ajili ya kufikishwa mbele ya sheria.
Wakati huo huo Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la
Suzane Mhendwa (45) mkazi wa kijiji cha uhamila Wilayani Mbarali ameuawa kwa
kuchomwa kisu kifuani baada ya kutokea kwa mzozo baiana yake na mtuhumiwa
nyumbani kwao.
Msangi alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana usiku majira ya saa 1:00 katika
kitongoji cha CCM Wilaya ya Mbarali ambapo marehemu alikuwa na mzozo na mtu
anayedaiwa kuwa ni ndugu yake na nipo alipochomwa kisu na kufa papo hapo na kwamba chanzo cha mauaji hayo
kinachunguzwa na mtuhumiwa anatafutwa
0 comments:
Post a Comment