Mbeya. Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule
Sekondari NzondaHaki ya jijini Mbeya na mkazi wa Nzovwe jijini hapa,
amefariki dunia baada ya kupigwa na jiwe kichwani.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakaeli
Masaki alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Joshua Buku (19) na kwamba ilidaiwa
kuwa alipgwa jiwe kichwani na kijana mmoja aliyetajwa kwa jina la Joshua Sadi
(17) mzaki wa Simike wote wa jijini Mbeya.
Kamanda Masaki alisema kuwa tukio hilo lilitokea
juzi saa 11:00 jioni eneo la Shule ya
Sekondari ya St, Marts iliyopo eneo la Forest Mpya, ambapo tukio hilo
lilisababishwa na ugomvi baina ya marehemu na mtuhumiwa wakati walipokuwa
wakicheza mpira wa miguu ndipo mtuhumiwa
akampiga kwa jiwe kichwani na kumjeruhi.
Alisema kuwa marehemu alifariki dunia wakati
akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya, na kwamba mtuhumiwa
amekamatwa na mwili wa marehemu huyo hadi jana ulikuwa umehifadhiwa hospitalini
hapo.
Awali, ilielezwa kuwa marehemu na mtuhumiwa walikuwa
wakisoma shule moja lakini mtuhumiwa aliacha masomo akiwa kidato cha tatu mwaka
jana.
Wakati huo huo, Kamanda Masaki alisema kuwa mfanyabiashara
na mkazi wa Chang’ombe kitongoji cha
Mwagala wilayani Chunya, Steven Daison (33) alivamiwa akiwa nyumbani kwake na
watu wanne na kumjeruhi kwa kumkata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na
kisha kumpora vitu vyake vikiwemo simu na fedha taslimu.
Kwa mujibu wa Kamanda Masaki , Daisoni aliwafahamu
watu hao kwa sura na kwamba tukio hilo lilitokea juzi usiku wa saa 7:00, ambapo
mbali na kumkatakata kwa mapanga pia aliporwa fedha kiasi cha Sh 1,800,000 simu pamoja na vocha za simu zenye thamani ya Sh1,200,000.
Kamanda Masaki alisema kuwa kabla ya tukio hilo watu
hao walifyatua risasi hewani na ganda
moja la risasi la aina ya Short Gun liliokotwa eneo hilo.
Alisema kuwa polisi wanendelea kuwasaka wahusika na
tukio hilo popote walipo ili waweze kutiwa nguvuni na mwathirika na tukio hilo
amepatiwa matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani kwake.
0 comments:
Post a Comment