Mkuu wa Wilaya Kyela Mkoani Mbeya Magreth Malenga akipokea gunia la mchele kutoka kwa Afisa mfawidhi Mkoa wa Mbeya wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF)Said Kipindura wakati wa kukabidhi msaada wa chakula wenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya Wahanga wa mafuriko Wilayani humo.
Afisa mfawidhi wa Mkoa wa Mbeya wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF)Said Kipindura akiwa amebeba ndoo za mafuta ya kula akizipeleka stoo wakati wa kukabidhi msaada wa chakula wenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya Wahanga wa mafuriko Wilayani
Zaidi ya Sh4.5bilioni zinahitajika kwa ajili ya kufanya matengenezo
ya miundombinu ya barabara na shule yaliyoharibiwa na mvua na kusababisha
kutokea kwa mafuriko katika Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Malenga mara baada ya
kupokea msaada wa chakula kutoka
mfuko wa pensheni kwa watumushi wa Umma(PSPF)wenye thamani ya Sh10milioni kwa ajili ya wahanga
wa mafuriko.
Alisema kuwa kutokana na mafuriko hayo barabara za halmashauri
ya Wilaya zimeharibiwa vibaya ikiwa ni pamoja na zile zilizopo chini ya wakala
wa barabara Tanzania (Tanroad)ambapo matengenezo ya haraka yanahitajika kwa
ajili ya kurudisha mawasiliano kama ilivyo awali.
Mkuu huyo alisema kuwa kutokana na uharibifu huo zaidi ya Sh2.3bilioni ambapo kwa upande wa
shule za msingi nane na moja ya Sekondari
zinahitajika zinahitajika Sh2.3bilioni kwa ajili ya matengenezo na kurudisha katika kazi yake ya awali.
“Kutokana na mafuriko hayo kuna changamoto nyingi ambazo
tunakabiliwa nazo katika masuala ya elimu kwani hata maabara ya baadhi ya shule
zetu zimeharibiwa vibaya na hivyo kusababisha wanafunzi wa kidato cha nne
kushindwa kufanya mazoezi ya vitendo katika mtihani wao wa mwisho kwa baadhi ya
shule”alisema
Alisema kuwa jumla ya kaya 3983 zenye watu 18,976 ziliathiliwa na mafuriko
hayo na kwamba kaya 235 zenye idadi
ya watu 1087 ndiyo zimefikiwa ambapo mifugo zaidi ya 3000 ilisombwa na
maji.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Afisa
mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Mbeya Said Kipindura
alisema kuwa mfuko huo umetoa kilo 4800
za mchele,maharagwe kilo 2000 na mafuta ya kula lita 600 ambavyo vyote vinathamani
ya Sh10milioni.
Kipindula alisema kuwa
mfuko huo unatambua kuwa unawajibu wa
kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidiana na
serikali katika kuisaidia jamii mara inapokuwa imekumbwa na
maafa.
0 comments:
Post a Comment