Pages

Friday, March 28, 2014

Safari ya hatari ya Mwandishi kwenda shule ya msingi Yala

Mwandishi akivuka  Mto Luswisi chini ya ulinzi wa Wenyeki wa kijiji cha Yala mara baada ya kunusurika kuliwa na Mamba katika safari yake ya kwenda shule ya msingi Yala
Mwandishi akivuka mto wa nne maarufu kwa jina la Luswisi ulio jirani na shule hiyo ya Yala  hapa ndipo alinusurika kuliwa na mamba  na kupata msaada kutoka kwa Wenyeji.

 Mwandishi akivuka mto wa pili


 Mwandishi akiendelea na safari yake ya kwenda shule ya msingi Yala
Baada ya kumaliza kuvuka mto wa pili

Mwandishi akiwa amefika katika shule ya Yala inayoonekana nyuma yake na hapa anajiandaa kuanza kuvuka mto Luswisi  uliojirani na  shule hiyo.

Mmliki wa mtandao huu Brandy Nelson baada kufanikiwa kuvuka mto wa pili  kati ya minne  katika safari yake ya kwenda shule ya msingi yala ambayo Wanafunzi na Walimu wa shule hiyo wanashindwa kufika shuleni hapo kwa ajili ya kuendelea na masoko wakati wa masika ambapo Mwandishi huyo alifanikiwa kufika shuleni hapo na kukuta hakuna Walimu na Wafunzi katika shule hiyo

Tuesday, March 25, 2014

Mwenyekiti wa Jumuia  ya watumia maji wa bonde dogo la  mto Kisongo ( Juwamaki) Mary Mwinuka akipokea meza na viti zilizotolewa na ofisi ya Bonde la ziwa Nyasa kwa ajili ya ofisi ya jumuia hiyo anayeshuhudia mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Juma Madaha.
Jumuia ya watumia maji wa mbonde dogo la mto Kisongo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mkoani NjombeJuma Madaha mwenye suti nyeusi katikati  mara baada ya uzinduzi wa jumuia hiyo wa kwanza kulia kwake ni Afisa wa maji wa bonde la ziwa Nyasa Witgal Nkondola,Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Wiliam Waziri na Mwenyekiti wa Juwamaki Mary Mwinuka
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Juma Madaha akimkabidhi pikipiki Mwenyekiti wa jumuia ya watumia maji katika bonde dogo la mto kisongo (JUWAMAKI)Mary Mwinuka iliyotolewa  na ofisi ya bonde la ziwa Nyasa.

Habari katika picha

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe akizindua rasimu ya katiba ya jumuia ya watumia maji katika bonde dogo la mto kisongo (Juwamaki)iliundwa na ofisi ya bonde la ziwa nyasa.