Pages

Tuesday, November 12, 2013

AFARIKI DUNIA KWA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI



AFARIKI DUNIA KWA KUNYWA POMBE  KUPITA KIASI

 Mkazi mmoja wa kijiji cha Masebe Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya  Anyimike Mwakyambo (54) amekutwa amefariki dunia ndani ya nyumba yake kwa kunywa pombe kupita kiasi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amesema kuwa tukio hilo lilitokea Nevemba 11,2013 majira ya saa 12:45 jioni  Marehemu  huyo anadaiwa kuwa alikunywa pombe kupita kiasi bila kula chakula.

Aidha Kamanda Athumani ametoa wito kwa jamii kuacha tabia yakunywa pombe kupita kiasi kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.

Na   Brandy Nelson



0 comments: