Pages

Monday, November 11, 2013

IRAN KUTOTELEKEZA HAKI ZAKE ZA NYUKLEA


Written By FURAHA ELIABU on Sunday | Sunday, November 10, 2013


RAIS Hassan Rouhani wa Iran amesema leo hii haki za nchi hiyo za kurutubisha madini ya urani ni mistari mekundu ambayo haiwezi kuvukwa na kwamba Jamhuri hiyo ya Kiislamu ilitumia busara wakati wa mazungumzo kuhusu mpango wa nuklea wa nchi hiyo.

Rais wa Iran Hassan Rowhani
Akizungumza katika bunge la taifa amesema wamewaeleza wajumbe wanaozungumza nao kuhusu mpango huo wa nuklea kwamba hawatosalimu amri kwa vitisho vyovyote vile,vikwazo, hila au kwa kubaguliwa na kwamba nchi hiyo haikuinamisha na haitoinamisha kichwa chake kutokana na vitisho kutoka mamlaka yoyote ile. 



Amesema kwamba kuna mistari mekundu ambayo haiwezi kuvukwa na maslahi ya taifa ni mistari mekundu yenye kujumuisha haki chini ya mifumo ya sheria za kimataifa na kurutubisha urani. 

Hapo jana Iran  na mataifa sita yenye nguvu duniani wameshindwa kufikia makubaliano ya kusitisha mpango wa nuklea wa Iran lakini yamesema tafauti zao zimepunguwa na wataanza tena mazungumzo katika kipindi cha siku 10 kujaribu kuumaliza mzozo huo uliodumu kwa muongo mmoja.
 
habari na Elimtaa

0 comments: