Mkuu wa Wilaya Chunya Mkoani Mbeya Deodatus Kinawiro akitoa maelekezo jinsi uwanja huo utakavyokuwa mbele ya Mtendaji mkuu wa kampuni ya saruji Mbeya (Lafarge)Catherin Langreney.
Mkuu wa Wilaya Chunya Mkoani Mbeya Deodatus Kinawiro akitoa taarifa ya ujenzi wa kiwanda hicho |
Mtendaji mkuu wa kampuni ya saruji Mbeya (Lafarge)Catherin Langreney akiteta jambo na mwandishi mkongwe wa michezo George Chanda |
Diwani wa kata Kiwanja akitoa salam katika hafla hiyo |
Mwenyekiti wa kijiji cha Mbugani Mungele akitoa salam katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa biashara wa kampuni ya Lafarge Mr.Mbaga akizungumza jambo katika hafla hiyo |
Jumla ya mifuko 1000 ya saruji sawa
na tani 50 yenye thamani ya Sh15milioni imetolewa na Kampuni ya saruji Mbeya (Mbeya cement) kwa serikali Wilayani
Chunya kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja
cha kisasa cha michezo Wilayani humo.
Ujenzi wa kiwanja hicho Chunya
unatarajia kugharimu kiasi cha fedha Sh 8bilioni ambapo tayari ujenzi wake umeanza
wilayani ambapo Uwanja huo wenye uwezo
wa kuchukua watazamaji 50,000 pia unatarajiwa kuwa kitega uchumi kwa halmashauri ya wilaya ya Chunya na mkoa wa Mbeya.
Akizungumza wakati wa kukabidhi saruji hiyo Mtendaji Mkuu wa Mbeya Cement Catherine Langreney alisema kuwa
kampuni yake imepokea maombi hayo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Chunya na kukubali
kuchangia saruji mifuko 1000 baada ya kugundua kuwa uwanja huo utaweza kutoa
ajira kwa vijana wengi na kuendeleza michezo.
Langreney alisema kuwa ksmpuni hiyo imekuwa ikichangia huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi
waliopo maeneo ya karibu na kiwanda hivyo, msaada huo ni sehemu ya huduma zao
za kawaida kwa wananchi.
Aidha alisema kuwa uongozi wa
kiwanda hicho unajipanga kutambulisha tekonolojia za kujenga nyumba bora kwa
gharama nafuu kwa lengo la kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chunya
Deodatus Kinawiro alisema kuwa uwanja huo unajengwa na wananchi wenyewe kwa
kushirikiana na Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo pendekezo la ujenzi wa uwanja
huo aliliwasilisha kwenye vikao vya halmashauri na kuridhiwa na baraza la
Madiwani.
Alisema katika vikao vyake, ambapo
Halmashauri ya wilaya hiyo ilipendekeza kutenga Sh 70milioni katika bajeti yake ya kila mwaka huku kila
mwananchi akiwajibika kuchangia ujenzi wa uwanja huo kuanzia sh.2000 kwa kila
mwaka ambapo matazamio uwanja huo unatarajia kukamilika 2016.
Alisema kuwa fursa ya kuwepo kwa
uwanja huo wa kisasa itainua michezo ndani ya wilaya hiyo na mkoa wa Mbeya kwa
ujumla hivyo wadau wanapaswa kujitokeza kuchangia maendeleo ya uwanja huo.
0 comments:
Post a Comment