Nahodha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Mbaspo Academy Boaz Mwire akipokea Kombe la kutoka kwa mgeni rasmi meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini Straton Mushi baada ya kushinda mabao 4 - 1 dhidi ya Elimu kutoka mbarali mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jiji mbeya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya pili.
Nahodha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Mbaspo Academy Boaz Mwire akiwakabidhi wenzake Kombe wachezaji wenzake baada ya kutwaa ubindwa kwa kushinda kwa mabao 4 - 1 dhidi ya Elimu kutoka mbarali mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jiji mbeya
Meneja wa Kampuni ya Artel kanda nyanda za juu kusini Staraton Mushi akisalimiana na wachezaji wa timu ya Elimu Kutoka Wilaya ya Mbarali |
Timu ya Mbaspo Academia ikiwa katika picha ya pamoja na Mmikili wa timu hiyo Seleman Harubu mwenye miwani na Meneja kampuni ya simu Airtel kanda nyanda za juu kusini Straton Mushi baada ya kunakua Kombe la Airtel Rising
Timu ya vijana ya Elimu kutoka Mbarali ikiwa tayari kwa ajili ya kukaguliwa
Timu ya Mbaspo Academy ya jijini Mbeya imetwaa ubingwa wa mashindano ya Airtel Rissing Stars ya 2014 chini ya miaka 17 baada ya kuifunga timu ya Elimu ya Wilayani mbarali mabao 4-1 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Timu hiyo ya Mbaspo imetwaa ubingwa huo kwa mara
ya pili mfululuzi ambapo mwaka jana pia ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa
kuifunga timu ya Wilayani Mbozi .
Katika
mchezo huo mabao ya Mbaspo yalifungwa na Richard Basyeti dk 6,Seif Gabriel dk
13,Joseph Shibanda dk 37 na Rafael Gondwe dk 78 wakati goli la toimu ya Elimu
lilifungwa na mchezaji wake Shaibu Mussa ambaye alifunga kwa penati dk ya 85.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi kombe hilo Meneja wa kampuni ya Airtel kanda nyanda za juu
kusini Straton Mushi alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kukuza soka la vijana
na kuweza kupata wachezaji wazuri
“Mashindano
haya yatakuwa endelevu ili kuhakikisha tunakuza soka la vijana na kuibua vipaji
ambavyo vitaisaidia TFF kupata timu nzuri ya Taifa na kuleta mwamko
kwa vijana kuendelea kuipenda soka”alisema
Alisema kuwa
vijana 16 waliochaguliwa katika
mashindano hayo watakwenda kupambana na vijana wengine kutoka mikoa ya
Ilala,Kinondoni,Temeke, Zanzibar,Mwanza
na Morogoro ambapo watachaguliwa vijana watakaounda timu ya Taifa ya
vijana ambayo itakwenda nchini
Garbon.
Kwa upande wake katibu wa chama cha Mpira Mkoa wa
Mbeya Seleman Harubu alisema kuwa katika mashindano hayo vijana 20 wamechaguliwa ambapo watachujwa na kupatikana vijana 16 watakaounda timu ya Mkoa.
0 comments:
Post a Comment