Askari polisi wakiwa katika eneo la Hospitali ya Rufaa Mbeya wakiwazia Chadema kubeba mwili wa marehemu huyo mkononi
Jeshi
la polisi Mkoani Mbeya limelazimika kutumia mabomu ya machozi kwa ajili ya
kuwazuia wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na
waombolezaji kuubeba mikononi mwili wa mwenyekiti wa serikali ya
mtaa wa Itiji Ezekiel King kwa tiketi ya chama hicho kwa lengo la
kutembea nao kwa miguu kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya hadi nyumbani kwake
Itiji.
Baada ya
mabomu hayo kurushwa viongozi na wafuasi wa chama hicho walilazimika kulibwaga
chini jeneza lililokuwa limebeba mwili wa marehemu na kulitelekeza na kuanza
kukimbia.
Marehemu
alifariki juzi katika hospitali ya rufaa Mbeya alikopelekwa kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua ghafla
katika gereza la Ruanda alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka Saba baada ya
kupatikana na kosa la kuzuru mwili .
Hatua ya jeshi la polisi kuamua kuchukua uwamuzi
huo ni baada ya viongozi na wafuasi wa Chadema kuuchukua mwili wa marehemu
kutoka chumba cha kuhifadha maiti katika hospitali ya rufaa huku mwili ukiwa kwenye toroli maalum la
kubebea wagonjwa na walipofika katika
geti hilo ndipo walipoubeba mkononi.
Baada ya
wafuasi hao kuubeba mwili huo mkononi ndipo mkuu wa polisi Wilaya ya Mbeya
(OCD)alipowazuia na kuwataka kutumia
gari kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kufanya maandamano.
Hali hiyo ya
mabishano ilisababisha kutokea kwa taharuki kubwa ambapo ghafla gari mbili
zilizokuwa zimewabeba askari kanzu na
askari wa kutuliza ghasia huku zikipeperusha bendera nyekundu zilipofika katika
eneo la mnara wa kumbukumbu ya mashujaa na kuwazuia kwa mbele na kuanza kurusha
mabomu ya machozi na kusababisha wafuasia hao kulibwaga chini jeneza lililokuwa
na mwili wa marehemu na kuanza kukimbia.
Askari
polisi waliokuwepo katika eneo hilo waliamua kulibeba jeneza hilo na
kulirudisha katika chumba cha kuhifadhia maiti na ndipo Mbunge wa jimbo la
Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (Sugu)alipowatuliza wafuasi hao kwa kuwataka
watulie kwani wanaenda kwenye kikao cha
pamoja na OCD kurishughulikia suala
hilo.
Akizungumza
mara baada ya kutoka kwenye kikao hicho Mbunge huyo alisema kuwa tayari suala
hilo wameshalizungumza na wamekubaliana kwa pamoja kuwa watabeba mwili huo kwa kutumia gari
lakini litakuwa likitembea kwa mwendo mdogo na wao bila kuwa na kelele za
shamlashamla
“Naomba
tuendelee kuwa na utulivu suala hili tumeshalizungumza limekwisha na
tumekubaliana kuwa askario wote waliopo hapa waondoke na magari yao na siosi
tutauchukua mwili wa marehemu na kuuweka kwenye gari na litatembea polepole
huku na sisi tukiusindikiza kwa mguu hadi
katika kanisa la Romani Katoriki la mjini”alisema
0 comments:
Post a Comment