MWISHO wa ligi
daraja la Nne iliyoanza kutimua vumbi katika viwanja vya Izumbwe kata ya Igale wilaya
ya Mbeya Vijijini jana, wachezaji wataibuka na Jezi na mipira huku vipaji vya michezo
mingine vikiibuliwa.
Hayo yalisemwa
na mgeni rasmi aliyefungua ligi hiyo, Gordon Kalulunga, ambaye kitaaluma ni mwandishi
wa habari mkoani hapa.
Mmoja wa marafiki wa Kalulunga, George Kazumba, akizungumza na wananchi wa kata ya Igale Mbeya Vijijini juzi.
Mmoja wa marafiki wa Kalulunga, Ayas Yusuph(ASIA PRIN), akizungumza na wananchi wa kata ya Igale Mbeya Vijijini juzi.
Mratibu wa masuala
ya michezo wa marafiki wa Kalulunga, Ayas Yusuph(Asia), aliwatambulisha baadhi ya
marafiki walioongoza na na mwanahabari huyo ambaoni Peter Mwalulili, Akimu Mwalupindi,
Frank Paskal na George Kazumba, ambao wote waliahidi kufanikisha uendeshaji wa ligi
hiyo.
Mmoja wa marafiki wa Kalulunga, George Kazumba, akizungumza na wananchi wa kata ya Igale Mbeya Vijijini juzi.
Mmoja wa marafiki wa Kalulunga, Aimu Mwalupindi, akizungumza na wananchi wa kata ya Igale Mbeya Vijijini juzi.
Marafiki wa Kalulunga,
waliahidi pia kuwapatia mpira mmoja wanafunzi wa shule ya msingi Izumbwe, kama zawadi
ya shule na kwamba kila Jumamosi watakuwa wanafanya bonaza katika maeneo mbalimbali
ya wilaya hiyo na nje ya wilaya kama walivyofanya wiki zilizopita katika uwanja
wa shule ya sekondarui Mbalizi kata ya Utengule Usongwe, kwa kuhusisha michezo ya
kukimbiza kuku, riadha, mpira wa pete na michezo mingine.
Gordon Kalulunga, akizungumza na wananchi wa kata ya Igale, wilaya ya Mbeya Vijijin |
Alisema kutokana
na kupata taarifa fupi ya mahitaji ya uendeshaji wa ligi hiyo na uhitaji wa zawadi
wakati wa kufunga ligi itakayodumu kwa mwezi mmoja, atashirikiana na marafiki zake
mbalimbali ili kufanikisha ligi hiyo na zawadi pia.
“Mimi sina fedha
za kununulia mahitaji yanayohitajika, lakini ni na utajiri wa marafiki mkiwemo ninyi,
kwasababu mmeniona ni muhimu kwenu, nimehamasika na kuwaza upya kama kauli mbiu
ya marafiki wa Kalulunga, tutatimiza” alisema Kalulunga.
Alisema tayari
alikuwa amewasiliana na baadhi ya marafiki zake akiwemo Mbunge wa Jimbo la
Songwe, Philipo MulugonaMbungewavitimaalummkoa waMbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa,
ambao wamekubali kuchangia mahitaji hayo.
Kwa hisani ya Mtandao wa www.kalulunga.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment