Pages

Sunday, March 8, 2015

Matukio ya sherehe za siku ya mkulima katika kijiji cha Lumbe Wilaya ya Rungwe


 Meneja wa mradi wa kilimo hifadhi kutoka shirika la HRNS Webster Miyanda akitoa maelezo mafupi kuhusu kilimo hicho katika  sherehe za siku ya mkulima zilizofanyika katika kijiji cha Lumbe Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya ambapo asilimia 90 ya wananchi wakijiji hicho wameamua kutumia kilimo hifadhi na kuachana na kilimo cha kawada kwa ajili ya kuwa na uhakika wa chakula.

Matukio katika picha ya Ziara ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika kiwanda cha kukoboa kahawa (CMS)

MENEJA Mkuu wa  kampuni ya kununua na kukoboa kahawa ya CMS Yogeshi akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuwa akiwasili katika kiwanda cha kukoboa kahawa cha CMS Mlowo Wilaya ya ,Mbozi Mkoani Mbeya 

Tuesday, March 3, 2015

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya awaapisha Wakuu wa Wilaya Wapya

 Wageni waalikwa waliohudhuria hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wa Wilaya Wapya iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya jijini hapa.
 Pichani ni wakuu wa Wilaya ya za Mkoa wa mbeya

Monday, March 2, 2015

SAFARI LAGER NYAMA CHOMA YAFIKA KILELE MBEYA, TUMAIN BAR& LODGE WAIBUKA KIDEDEA.

 Mgeni rasmi katika mashindano ya safari lager nyama choma, Katibu tawala wa Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela, akizungumza na wakazi wa Jiji la Mbeya kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
 Meneja wa Bia ya Safari lager Edith Bebwa, akitoa neno la utangulizi kabla ya kuanza kukabidhi zawadi katika fainali ya nyama choma.

 Jaji Mkuu akitaja majina ya washindi
 Mgeni rasmi pamoja na watumishi wa TBL wakijiandaa kuanza kutoa zawadi.
 Mwakilishi wa mshindi wa kwanza ambaye ni Tumain Bar akionesha kombe juu
 Picha ya pamoja washindi wote pamoja na uongozi.
 Meneja wa bia ya safari pamoja na mkuu wa matukio Kanda wakifuatilia kwa makini mashindano ya kuchoma nyama.
 Watumishi wa TBL wakila nyama kwenye moja ya mabanda ya mashindano







 Wateja mbali mbali wakiwa wanapata huduma kwenye mabanda.

BAA ya Tumain iliyopo Ilomba jijini Mbeya imeibuka kinara wa kuchoma nyama katika Fainali iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Chuo cha Uhasibu Mbeya(TIA).
Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari yaliyojulikana kwa jina la Safari lager nyama choma 2015 yalishirikisha baa zaidi ya 20 ambapo baa tano zilitinga fainali.
Mshindi wa kwanza katika fainali hizo Baa ya Tumaini ilijinyakulia Kombe kubwa,Fedha taslimu shilingi Milioni Moja pamoja na Cheti maalumu.
Jaji Mkuu wa Mashindano hayo, Manase alisema mshindi amepatikana kutokana na vigezo ambavyo waliambiwa kwenye semina elekezi kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na usafi wa mazingira yanayochomewa nyama, usafi wa mchomaji mwenyewe,aina ya nyama anayopaswa kuchoma, mazingira kwa ujumla pamoja na utoaji huduma kwa wateja.
Aliitaja baa iliyoibuka msindi wa pili kuwa ni City Pub iliyopo Mwanjelwa iliyojipatia Cheti na fedha shiliki Laki nane, mshindi wa tatu Kalembo baa ya Sokomatola iliyojipatia cheti na shilingi laki sita, msindi wa nne  ni Samaki samaki aliyoibuka na Cheti pamoja na shilingi laki nne huku nafasi ya tano ikienda kwa Nebana  baa iliyopata Cheti na shilingi laki mbili.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika fainali hizo, Quip Mbeyela Katibu tawala Wilaya ya Mbeya, aliipongeza Kampuni  ya Bia TBL kuwa imekuwa ikijitahidi kushirikiana na serikali katika kutoa huduma na kuwawezesha wajasiliamali wadogo.
Aliongeza kuwa  pia Kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kulipa Kodi ambayo imekuwa ikiisaidia Serikali katika kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma kwa jamii.
Naye Meneja wa Bia Safari lager nchini, Edith Bebwa alisema fainali hizo zimeanzia mkoani Mbeya kutokana na wakazi wa Mkoa huo kuongoza katika Unywaji wa bia ya Safari.
Alisema baada ya hapo zoezi hilo litahamia katika mikoa mingine na kuongeza kuwa lengo la mashindano ni kuwawezesha walaji wa nyama wanapata kitu ambacho kimeandaliwa katika mazingira sahihi.
Kwa hisani ya Mbeya yetu Blog

AUA MKE WAKE NA KISHA KUJIUA

 Baadhi ya majirani wa mtaa wa Hayanga RRM jijini Mbeya wakiwa nje ya nyumba ambapo tukio hilo limetokea .

Watu wawili wafanyakazi  shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Mbeya Ndugu Uswege Mwankuge (58) na Jusio Uswege (48) ambao ni mtu na mke wake wamekutwa wamekufa ndani ya nyumba yao mtaa hayanga  RRM jijini mbeya .