Katibu wa CCM Mbeya mjini Kerenge akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya mjini Sambwee Shitambala katika mkutano wa kampeni wa Ubunge jimbo la Mbeya mjini kata ya Itezi |
Mwenyekiti wa CCM Mbeya mjini Ephrahimu Mwaitenda akizungumza na wakazi wa kata ya Itezi kwenye mkutano wa kampeni za Ubunge jimbo la Mbeya mjini |
Meneja Kampeni wa Mbunge wa Mbeya mjini Charles Mwakipesile akizungumza na wakazi wa Jimbo la Mbeya kata ya Itezi kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Sambwee Shitambala |
Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya mjini Sambwee Shitambala akizungumza na wakazi wa kata ya Itezi kwenye mkutano wa kampeni za Ubunge leo jioni. |
Mgombea Udiwani wa kata ya Itezi kwa tiketi ya ACT Bakari Hamisi akiuliza swali kwa mgombea Ubunge wa CCM kwenye mkutano wa kampeni leo jioni |
Na Ripota Wetu
WAKAZI wa kata ya Itezi jimbo la Mbeya mjini wamehakikishiwa kuwa mgombea Ubunge wa CCM jimboni humo Sambwee Shitambala akichaguliwa anayo nafasi ya kuwa Waziri kwenye serikali itakayoundwa na Dkt. John Magufuli.
Akizungumza wakati wa kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Meneja wa kampeni wa mgombea huyo Charles Mwakipesile aliwahakikishia wakazi wa Kata hiyo kuwa Shitambala anayo nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwa Waziri akichaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Alisema uwezo alionao Shitambala unaendana na hadhi ya Jiji hilo na kuwa ni vyema wakazi wa Jiji hilo wakathamini uwezo wake na kumchagua ili Jiji lipate heshima ya kuwa na Waziri kwenye serikali ya awamu ya tano itakayoundwa na Dkt. Magufuli.
Kwa upande wake Shitambala aliwahakikishia wakazi wa Jiji la Mbeya hasa vijana kuwa uwezekano wa wao kupata ajira bora utaendana na wao kukichagua Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa ndicho pekee chenye sera ya kuboresha maisha ya wananchi wake.
Alisema vijana wanayo nafasi kubwa ya kuwa na ajira bora kupitia sera za mgombea urais wa CCM Dkt. Magufuli ambaye ameahidi kufufua viwanda vilivyokufa.
Shitambala alisema kuwa njia pekee ya vijana kuishi kwa amani na utulivu ni kukichagua CCM ili kuepuka vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani na kuwa yeye atasimamia kuwepo kwa amani na salama na vijana kujishughulisha zaidi na mambo ya maendeleo badala ya vurugu.
Kampeni za uchaguzi mkuu zinaendelea katika maeneo mbalimbali jijini Mbeya huku wagombea wakiendelea kunadi sera zao kwa wananchi ili kuchaguliwa kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment