LIGI
kuu ya Vodacom imeendelea leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine
ulipozikutanisha timu za Mbeya City na Simba ya Dar es salaam ambapo kwa
mara ya kwanza imevunja mwiko na kuichapa Mbeya City bao 1-0.
Tangu
timu ya Mbeya City ipande daraja mwaka juzi haijawahi kufungwa na Simba
katika uwanja wake wa nyumbani na mara ambapo katika msimu uliopita
Simba ilifungwa nyumbani na ugenini.
Goli
la kuvunja mwiko la Simba lilipatikana dakika ya 2 ya mchezo ambalo
lilifungwa na Murshid Juuko kwa kichwa baada kona iliyopigwa na Mohamed
Husein ambapo mpira ulitua kichwani kwa Murshid na kuusindikiza wavuni
huku golikipa wa Mbeya City Juma Kaseja akichupa bila mafanikio.
Hadi
kipindi cha kwanza kinamalizika Simba walikuwa kifua mbele kwa bao
1-0.Kipindi cha pili kwa timu ya Mbeya City kuonesha makeke langoni mwa
Simba lakini washambuliaji wa timu hiyo walikosa ushirikiano na hivyo
kujikuta wakishindwa kuliona lango la Simba.
Walinzi
wa Simba Hassan Ramadhan, Said Hamis,Mwinyi Kazimoto, Justice Majabvi
alijitahidi kuondosha hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni mwa timu
yao ambapo washambuliaji wa Mbeya City Hamad Kibopile,Christian Sembuli,
Themi Felix, Geofrey Mlawa na Rafael Alpha walionekana kukwaa
kizingiti.
Hadi kipyenga cha dakika tisini kinapulizwa Simba walitoka kifua mbele kwa bao 1-0.
Baadhi
ya wapenzi na mashabiki wa timu ya Mbeya City wamedai kuwa kocha mpya
wa Mbeya City Majao Mingange ana kazi ngumu ya kurejesha hamasa za
wachezaji wake hasa baada aliyekuwa kocha wa timu hiyo Juma Mwambusi
kuhamia timu ya Yanga.
Kocha
Mwingange ambaye awali alikuwa akikinoa kikosi cha Ndanda ya Mtwara
alisema kuwa kazi aliyonayo si kubwa sana kwa wachezaji wake na kuwa
yapo marekebisho madogo ambayo yakifanyiwa kazi wachezaji hao wataonesha
kabumbu safi katika michezo ijayo.(STORI/PICHA KWA HISANI RASHID MKWINDA)