Dar
es salaam,Ikiwa ni jitihada mahususi kuwapa
saruji imara zaidi wakandarasi na wafyatuaji matofali Lafarge Tanzania imezindua
chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” ambayo ni imara na mahususi
kwa ufyatuaji matofali, zege, majengo makubwa pamoja na miradi mikubwa ya
miundombinu kama madaraja, barabara na majukwaa ya michezo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo leo, Afisa Mtendaji Mkuu
wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney alisema kwamba Tembo Supaset 42.5 ni saruji
maalum iliyobuniwa ili kukidhi ongezeko kubwa la mahitaji ya saruji imara na
inayokauka haraka katika soko la ufyatuaji matofali na zege na ujenzi mkubwa “Tembo
Supaset ni matokeo ya utafiti makini uliofanywa na wataalamu wetu na
imetengenezwa mahususi kukidhi mahitaji ya soko.”alisema.
Akizungumzia kuhusu maendeleo katika sekta ya ujenzi
Langreney alisema kwamba kwa ujumla thamani ya sekta ya ujenzi nchini Tanzania
inakadiriwa kuwa dola bilioni. Sekta hiyo ilikua kwa asilimia 7.8 mwaka 2014 na
ni sawa na asilimia 8.6 ya pato la taifa ikiwa ni kutokana na ujenzi binafsi, usafirishaji
na miradi mikubwa ya ujenzi. Tanzania ina idadi ya zaidi ya milioni 44 kufikia
mwaka 2014 na inatarajiwa kuongezeka sambamba na ongezeko la mahitaji ya nyumba
na miundombinu.”
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan
Chonjo alisema kuwa Tembo Supaset ambayo itauzwa kwenye soko la jumla na
rejareja ikiwa katika ujazo wa kilo 50 ni saruji imara zaidi ikiwa na ubora
kuliko saruji nyingine zilizopo kwenye soko kutokana na uimara pamoja na bei shindani
ambazo zimepangwa na itakidhi mahitaji ya watumiaji kama vile:
- Kuimarika mapema jambo ambalo litawaongezea tija wazalishaji bidhaa zinazotokana na zege
- Ukaukaji wa haraka jambo litakaloyafanya matofali yaweze kuhamishika haraka na kuongeza tija wazalishaji
- Mchanganyiko mzuri wa zege na matumizi kidogo ya maji kuimarisha.
Chonjo alisema kwamba Tembo
Supaset imezinduliwa ili kukidhi mahitaji ya soko kuwa na saruji imara zaidi
huku akitarajia saruji hyo kupanua soko la Lafarge Tanzania hususani kwa
wafyatuaji ambao hutegemea saruji inayoimarika haraka katika kazi yao. “Mbali
na uimara, faida nyingine ya Supaset ni kuweza kudumu kwa muda mrefu ikiwa na
maana kwamba majengo yatakayojengwa kwa saruji hiyo yatadumu zaidi”
Alisema neno Supaset linamaanisha uimara kutokana na
kukauka mapema na kukaa muda mrefu zaidi katika uimara na saruji hiyo ni sehemu
ya saruji za chapa ya Tembo.
0 comments:
Post a Comment