Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lafarge Tanzania Ilse Boshoff akizindua saruji mpya ya Tembo Fundi maalumu kwa ajili ya mafundi waashi |
Mkurugenzi Mtendaji wa Lafarge Tanzani Ilse Boshoff akiwa pamoja na baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa Kampuni hiyo |
Kampuni ya Saruji Lafarge Tanzania imezindua
saruji ya kwanza maalumu kwa matumizi ya uashi. Saruji hii inayojulikana kama
Tembo Fundi itawapa wajenzi chaguo bora kwa ajili ya kazi za uashi ikiwa ni
pamoja na kupiga plasta ukuta, kusakafia, kujengea tofali na kupangilia
marumaru.
Saruji hiyo iliyotengenezwa maalum
kwa kazi ya uashi wa kuta za nje na ndani ina ubora katika kufanya kazi, nguvu
kwenye ugundishaji inashika vizuri na ina umaliziaji bora wenye kuleta matokeo
yaliyo
bora zaidi kwenye kujenga tofali,
uzio, marumaru na sakafu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo,
Ilse Boshoff, alisema wakati wa uzinduzi leo kwamba Tembo Fundi imeundwa
mahususi kwa ajili ya kazi za uashi na kuwapa wajenzi utendaji bora wa kazi na
thamani ya fedha.
“Ikiwa imetengenezwa kutokana na
uzoefu na utaalamu wa Lafarge kimataifa katika kuzalisha saruji, Tembo Fundi ni
rahisi kutumia katika kupiga plasta, tofauti na saruji ya matumizi ya jumla
ambayo itamchukua muashi muda mrefu katika kusawazisha ukuta.
Alisema faida nyingine muhimu katika
matumizi ya Tembo Fundi ni unafuu katika gharama kutokana na mfuko mmoja wa
Tembo Fundi kutumika eneo pana zaidi ukilinganisha na mfuko wa saruji ya
matumizi ya jumla. Kutokana ya kwamba inafanya kazi vizuri na uimara wake
kudumu kwa muda mrefu Tembo Fundi itawasaidia wajenzi kupunguza gharama kwa
kiasi kikubwa.
LAFARGE TANZANIA
Mbeya Cement Co. Ltd | Oyster Plaza,
3rd Floor | Plot 1196 Haile Selassie Road
P.O. Box 46452 | Dar Es Salaam -
Tanzania - ( office +255 222 923 300\1
Songwe Industrial Area | Tunduma
Highway
P.O. Box 529| Mbeya – Tanzania ( office +255 252 950 005/6
0 comments:
Post a Comment