Kiongozi wa timu ya Uzinduzi Dkt.Peter Kilima akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya Uimarishaji Mifumo ya Sekta za umma |
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Richard Moshi akitanganza Halmashauri mbili za mwanzo zilizochaguliwa kushiriki mafunzo ya Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma kwa madiwani. |
Mkurugenzi Msaidizi, Uismamizi Rasilimali watu Ofisi ya Rais TAMISEMI Miriam Mmbaga akitoa nasaha mara baada ya kufungwa kwa uzinduzi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma mjini Njombe. |
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma wakiwa kwenye kazi za vikundi |
Kiongozi wa Timu ya Uzinduzi Dkt Peter Kilima akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari |
Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Assumpter Mshama akizungumza kwenye kikao kilichozishirikisha Halmashauri 6 za Mkoa wa Njombe |
HALMASHAURI
2 za Makete na Wanging’ombe mkoani Njombe zimechaguliwa kuingia katika awamu ya
kwanza ya mafunzo ya Uimarishaji Mifumo
ya Sekta za Umma (PS3).
Mafunzo hayo
yanayofadhiliwa na Shirika la Msaada la Kimataifa la Marekani USAID yatawahusisha
Wenyeviti wa Halmashauri,Wakurugenzi pamoja na wakuu wa Wilaya.
Akizungumza
mara baada ya kutangazwa kwa Halmashauri hizo Kiongozi wa timu ya Uzinduzi Dkt
Peter Kilima alisema Halmashauri hizo zimechaguliwa kuwa za mwanzo kushiriki
mafunzo hayo kutokana na changamoto walizonazo.
‘’Vigezo vya
uhitaji vimewapa nafasi ya kwanza kushiriki mafunzo haya kwa Madiwani ingawa
halmashauri zote za Mkoa wa Njombe zitapata mafunzo hayo kwa awamu ya pili’’
Alisema
mafunzo hayo yanatarajia kuanza Jumatatu ijayo mjini Njombe na kutolewa na
wataalamu wa mafunzo kutokea mjini Dodoma.
Akizungumzia
kuteuliwa kwa Halmashauri ya Makete,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Egnato Mtawa
alisema anaamini changamoto zilizopo zimetoa kipaumbele kwao kuwa wa mwanzo
kupata mafunzo hayo.
‘’Changamoto
za Wilaya yetu zimetupa kipaumbele kuteuliwa wa mwanzo kupata mafunzo kwa
Madiwani,tuna changamoto za jiografia na Miundo mbinu, tunaamini hatimaye changamoto
tulizonazo zitapatiwa ufumbuzi’’ alisema Mtawa.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Assumpter Mshama alisema mafunzo hayo kwa
Madiwani yataongeza weledi wa utendaji kazi kwa watumishi kutokana na Halmashauri hiyo kuwa mpya.
Awali
akizungumza mara baada ya kufungwa kwa uzinduzi huo Mkurugenzi Msaidizi,
Usimamizi wa Rasilimali watu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Miriam Mmbaga alisema
kukosekana kwa maadili kwa watumishi wa umma ndiko kunakosababisha Halmashauri
nyingi zipate hati zenye mashaka.
Alifafanua
kuwa maadili yanayoelezwa ni yale yale yaliyopo katika imani za dini kwa kuwa
vitabu vya dini zote zinapinga vitendo viovu ikiwemo rushwa.
‘’Dini zote
zinapinga rushwa, maadili ya utumishi wa umma ni yale yale yaliyopo kwenye
vitabu vya Uislamu na Ukristo,’’ alisisitiza.
0 comments:
Post a Comment