Pages

Saturday, June 18, 2016

MAKALLA ASHIRIKI UJENZI WA KITEPUTEPU RUNGWE



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipita kwenye eneo la kivuko cha Kibundungulu kilichopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambacho kinajengwa

Mkazi wa kijiji cha Kibundungulu akipita ndani ya mto Mbaka kutokana na kivuko cha eneo hilo kuvunjika baada ya kutokea mafuriko wakati wa masika

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akishiriki kukoroga zege kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha Kibundungulu wilayani Rungwe

Mkuu wa mkoa wa Mbeya akizungumza na wakazi wa eneo la mto Mbaka ambako kinajengwa kivuko

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kivuko katika mto Mbaka wilayani Rungwe

Kilio cha wakazi wa kitongoji cha Kibundungulu kilichopo katika kijiji cha Mbaka wilayani Rungwe waliokuwa wakipata tabu kuvuka kwenye kiteputepu sasa kumalizwa mwezi ujao.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla ambaye amewatembelea wananchi wa kitongoji hicho na kushiriki ujenzi wa kivuko hicho jana amesema kitengo cha Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kimemuwezesha Mkandarasi kukamilisha kivuko hicho kwa muda wa wiki mbili.
Amesema kwa mujibu wa mkandarasi kivuko hicho kitakamilika Julai 8 na wananchi wa kijiji hicho wataanza kupata huduma muhimu za kijamii kwa kutumia kivuko hicho.
Awali wananchi wa maeneo hayo walikuwa wakipita ndani ya mto kutokana na kivuko hicho kusombwa na maji wakati wa masika na kwamba kivuko hicho kitakuwa ni cha muda huku kukiwa na mkakati wa kujenga daraja la kudumu.
Aidha Makalla amewasihi wananchi kuacha kuvuka kwa kutumia waya na kuwa kukamilika kwa kivuko hicho kitasaidia wananchi kuondokana na tatizo la kuvuka kwenye mto wenye maji mengi jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao.

0 comments: