“Nilipata ajali ya kudongoka kutoka juu
ya mti hadi chini na kuvunjika kiuno wakati nikiwa katika harakati za kuokota
kuni na ndiyo sababu ya kulazwa hapa hospitalini kwa muda wa miaka 14 sasa kwa
ajili y kuapata matibabu”
Hiyo ni kauli ya Lines
Mwamlima (43) mkazi wa kjji cha Igale Wilaya ya Mbeya vijini akiwa katika
hospitali ya Mission ya Mbozi Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya
inayomilikiwa na kanisa la Moraviani jimbo la kusini Magharibi
alipiokuwa akiongea na Mwandishi wa makala haya hospitalini hapo.
Lines ambaye ni mwanamke
mjane baada ya mume wake alifariki dunia kwa ajali
mwaka 1998 na kumuachia watoto wanne anasema kuwa alipata ajali ya
kuanguka kutoka juu ya mti hadi chini mwaka 1999 na kusababisha kuvunjika
kiuno na kupata madhara makubwa katika uti wa mgongo.
“ilikuwa ni kawaida yangu kutoka
nyumbani asubuhi na kwenda msituni kutafuta kuni kwa ajili ya matumizi ya
nyumbani na kurudi nyumbani salama lakini siku ile ilikuwa siku ya
uchungu ambayo sitoweza kuisahau maishani mwangu “anasema
Anasema kuwa baada ya kufika katika
msito huo uliopo mbali kidogo na nyumbani kwake alipanda juu ya mti kwa lengo
la kukata vimiti vidogo vidogo vilivyopo kwenye matawi ya mti huo ndipo alipoteleza
na kuanguka chini .
“Baada ya kupata ile ajali nililia
kwa uchungu na ndipo wasamalia wema waliposikia sauti za kilio changu
wakaja kuniangalia nakunikuta nimelala chini huku nikilia kwa nguvu kutokana na
maumivi makali niliyokuwa nikioyapata na ndipo walipoamua kunikimbiza na
kunileta hapa hospitalini”anasema
Anasema kuwa baada ya kufika
hospitalini hapo alipatiwa huduma ya kwanza na kwamba baada ya vipimo
madaktari walimpa kibali cha kwenda kutibiwa katika hospitali ya Taifa
Mhimbili kwa kuwa hospitalini hapo hakuna vifaa vya
kuunghanisha mifupa yote ya uti wa mgongo .
“Walidai pia kuwa nilikuwa na
TB ya uti wa mgongo na ndipo nilipoangukia hivyo wakasema kuwa hawana
vifaa vya kuunganisha mifupa ya uti wa mgongo na baada ya kukaa mwezi
mmoja hapa nikapelekwa muhimbili mwezi Mei 1999”anasema
Anasema kuwa baada ya kufika
muhimbili alifanyiwa uchunguzi na kubaini kuwa alikuwa na TB ya uti wa
mgongo ambapo walianza kumpa matibabu ya TB ya miezi sita “ambapo
katika hospitali ya muhimbili nilikaa muda wa miezi mitano nakurudi hapa
tena kwani waliniuliza kama nina ndugu naweza kuendelea kukaa hapo kwa
mika watakayonipamgia lakini nilikataa baada ya kuona sina ndugu yoyote na sia
uwezo kifedha wa kuishi jijini Dar es salaam”anasema
Mwamlima anasema kuwa
baada kukataa alirudiswa katika hospitali hiyo ya Mbozi Mission
mwaka 2000 na kuanza kuendelea kupata matibabu madogodogo “lakini nilitokwa na
vidonda kwenye makalio na mgongoni kutokana na kulala kwa muda mrefu”anasema
Anasema kuwa alikaa hospitalimi hapo
kwa muda wa miaka tisa na ndipo alipoomba kurudishwa nyumbani kwake kutokana na
kuwakumbuka watoto wake ambapo madakatari wa hospitalini hapo walikubali
kumrudisha nyumbani kwake.
“Baada ya kurudi
nyumbani hali ilikuwa ni mbaya sana na ndipo Dk Charles Mbwanji alipokuja
kunitembelea akanikuta hali yangu ni mbaya sijiwezi kwa lolote na mama
yangu ni mzee hana uwezo wa kunihudumia kwani nilikuwa nahitaji
mtu mwenye nguvu kwa ajili ya wa kunigeuza hivyo Dk Mbwanji akanirudisha hapa
hospitali “anasema
Anasema kuwa awali
katika hospitali hiyo walikuja madaktari Wazuingu ambao walikuwa wamfanyisha
mazoezi na kufanikiwa kuweza kukaa lakini madakakrati hao
walipoondoka hakuweza kupata huduma hiyo tena na hali yake kuendelea
kama ilivyo awali.
Anaeleza kuwa kwa sasa
miguu yake haina nguvu,hawezi kutembea na kwamba hakuweza kupata hedhi ndani ya
miaka sita na kwamba anaendelea kupata matibabu madogomadogo katika
hospitali hiyo lakini bado anahitaji matibabu zaidi.
“Nahitaji kupata msaada wa matibabu
zaidi kwani ninaamini kuna hospitali kubwa ambazo zinawataalamu wa uti wa
mgongo na kiuno kwani mimi sina uwezo ndugu wa kunifatia hizo
hospitali wala fedha kwani ndugu niliyebaki naye huyu mama yangu
ambaye ni mzee ambaye alikuwa ni mkulima lakini kwa sasa hana nguvu za kulimia
yupo hapa hospitalini kwa ajili ya kusaidia ninapokuwa nahitaji kupata
haja kubwa na ndogo na kunipikia chakula”anasema
Akielezea hali ya mgonjwa huyo kwa
sasa Dk Charles Mbwanji anasema kuwa baada ya kupelekwa katika hospitali
ya muhimbili ilibainika kuwa ugonjwa huo hauwezi kupona.
“Huyu mgonjwa hawezi kupona tena
kwani ndivyo taarifa ya kutoka katika hospitali ya Taifa ya muhimbili kutokana
na ajali alivyoipata hivyo amepooza kuanzia kiunoni hadi miguuni”alisema
Anasema kinachomfanya kuwepo muda
mrefu katika hospitali hiyo ni kutokana na kuwepo kwa mazingira magumu nyumbani
kwao na hana mtu wakumuuguza na kwamba uongozi wa hospitali hiyo ulikubaliana
na kumuacha aendelee kukaa hospitalini hapo .
“Akikaa hapa hospitalini hali yake
inakuwa nzuri kwani anapata matibabu kwa ukaribu na sasa kinachomsumbua
ni homa,vidonda katika sehemu ya makalio vilivyotokana na kulala kwa muda
mrefu na kutumia mpira wa mkojo kwa muda mrefu na hivyo kumsababishia kupata
ugonjwa wa UTI mara kwa mara na siku zake za hedhi kuwa nyingi kupita
kiasi”anasema
Kwa upande wake muuguzi msaidizi wa
hospitali ya Mbozi Mission Peter Kamendu anasema mama huyo
anasumbuliwa nma tatizo la kufa kwa viungo vya mwili (Paraptegia) ambapo
ajali aliyoupata ilisababisha viungo vyake kuanzia kiunoni hadi miguuni
kushindwa kufanya kazi.
“Tulimpokea huyu mama mwaka 1999
baada ya kupata ajali hiyo kama alivyooleza mwenyewe lakini hospitali
tumeona siyo vizuri kuacha akae nyumbani kwake wakati bado tatizo lake ni kubwa
na anahitaji msaada wa karibu kutoka kwa wataalam”anasema
Naye mama mzazi wa Lines
Zaituni Mgunji (80) anasema kuwa uumia kwa mtoto wake limekuwa pigo kubwa
kwakwe kwani hana uwezo kifedha wa kumhudumia mtoto wake kwa ajili ya
kupata matibabu zaidi ili kufanikiwa kurudi katika hali yake ya zamani
kutokana na umasikini aliokuwa nao.
“Hata hivyo naushukuru uongozi wa
hospitali hii ya Mbozi Mission kwa kuniruhusu kukaa hapa na mtoto wangu
katika kipindi cha miaka 14 bila kutoa malipo yoyote kweli mungu ni
ajabu kwani sijawahi kuona wala kusikia muujiza kama huu wa
hospitalia ya Mission ya Mbozi”anasema
Anasema kuwa kwa sasa hana uwezo
kifedha “kwani sina uwezo wa kulima tena nguvu zimekwisha mwanangu hivyo
hata chakula naomba kwa wasamalia Wema ndiyo wananisaidia chakula kwa ajili
yangu na mtoto wangu huyu mgonjwa”anasema
Na Brandy Nelson
0 comments:
Post a Comment