Pages

Tuesday, November 12, 2013

WAGONJWA WA KIFUA KIKUU WAONGEZEKA MBEYA






Machi 24 ni siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa kifua kikuu  ambapo watu wote duniani wameadhimisha siku hiyo  huku  Mkoa wa mbeya  ukiadhimisha  ukiwa na changamoto ya ongezeko la Wagonjwa wa kifua kikuu .

 Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na vimelea viitwavyo Mycobacterium Tuberculosis ambapo kinaambukizwa kwa njia ya hewa kutoka kwa mgonjwa mwenye kifua kkuu kwenda  kwa watu wengine.

Hali ya maambukizi ya ugonjwa huo hutokea hasa katika sehemu zenye msongamano wa watu au nyumba  ambazo hazipitishi hewa na Mwanga wa kutosha.

Kifua kikuu huigundulika kwa njia kuu ya kupima vimelea kwenye makohozi n kwa kuumia Darubini,na njia zingine ni kwa kupiga picha za X-ray na Gene X  Part na kwamba wanasayansi  wanazidi kufanya utafiti juu ya njia nyingine mbadala za kuundua kifua kikuu zilizo rahisi na haraka zaidi.

Katika maadhimisho ya siku ya ukimwi mwaka huu  2013 kauli mbiu ilikuwa “JUKUMU LA KUDHIBITI KIFUA KIKUU NI LA KILA MMOJA WETU”ambapo  jamii kwa ujumla ina wajibu wa kudhibiti kifua kikuu  kwa kufuata maelekezo ya Waatalm.

Hali ya kifua kikuu

Zaidi ya asilimia 30 ya watu  Duniani wameambuikizwa kifua kikuu  huku Tanzania ikiwa ni nchi ya 18 kati ya nchi 22 zenye Wagonjwa wengi Duniani ambapo idadi ya watu wenye kifua kikuu Tanzania imeongezeka kwa haraka kutoka watu 11,000 mwaka 1984 hadi watu 62,000 mwaka 2006 na Wagonjwa 63,453 kufikia mwaka 2010.
Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma Mkoa wa Mbeya  Dk Yesaya Mwasubira  anaeleza kuwa Mikoa yenye idadi kubwa ya Wagojwa wa kifua kikuu kufuatiwa Takwimu za Mwaka 2010 kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma (NTLP) ni pamoja na Mkoa wa Mbeya .

Anasema kuwa kati ya mikoa 10 yenye wagonjwa wengi wa kifua kikuu Mbeya ni moja wapo ikishika nafasi ya sita kwa kuwa na sailimia 5.1 ikifuatiwa na Iringa (5.0),Arusha (4.4)Mara (4.3),Manyara (4.1) na asilimia 29.2 kwa mikoa inayobaki huku mkoa wa Dar es salaam ukuiongoza kwa kuwa na asilimia 21.2 na kufuiatiwa Mwanza (8.9)Shinyanga(6.7) Morogoro (5.9) na Tanga asilimia 5.3.

“Kwa Mkoa wa Mbeya  Wagonjwa wamekuwa wakiongezeka mara kwa mara na kutokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na maambukizi  mapya ya virusi vya ukimwi  pamoja jamii kutambua umuhimu wa kupambana na maambukizi ya ugonjwa  wa kifua kikuu”anasema

Anasema kuwa katika Mkoa wa Mbeya wagonjwa wameongezeka  kutoka 3743 mwaka 2000 hadi wagonjwa 3952 mwaka 2005 na kwamba baada ya wagonjwa walipungua hadi kufikia 2949 mwaka 2008.

Dk Mwasubira anasema kuwa  iadio hiyop ilianza kuongezeka kwa mara nyingine ambapo  mwaka 2009 wagonjwa walikuwa 3110,mwaka 2010 wagonjwa 3215, huku mwaka 2011 walikuwa wagonjwa 3418 na mwaka 2012 walifikia wagonjwa 3502.

“Takwimu za mwaka 2011 zinaonyesha kila  watu 100,000 Mkoani Mbeya  watu 127 hupatikana kuwana kifua kikuu kwa mwaka na watu 129 kwa kila watu 100,00 kwa mwaka 2012 hizi takwimu zinaonyesha dhahiri kuwa idadi ya Wagonjwa wa kifua kikuu inazidi kuongezeka kila mwaka katika Mkoa wa Mbeya”anasema

Hali ya kifua kikuu kwa Wilaya za Mkoa wa Mbeya  kwa mwaka 2012 takwimu zionaonyesha  jiji la Mbeya  linaonyesha kuwa na Wagonjwa wengi wa kifua kikuu ikifiwatiwa na Mbrali,Mbozi,Rungwe,Kyela,Chunya,Mbeya na Ilejena kwamba asilimia 98 ya Wagonjwa wakifua kuku wanaopata matibabu ma kumaliza matibabu hupuna kabisa.

Virusi vya ukimwi na kifua kikuu

Anaeleza kuwa  virusi  vya ukimwi vimeongeza kasi ya ongezejko la kifua kikuu seheu ya  nyingi Duniani ikiwemo Mbeya  na kwamba kifua kikuu kinasababisha  vifo miongoni mwa wenye virusi vya ukimwi.

Anasema kuwa kwa Mkoa wa Mbeya  takribani asilimia 60 ya Wagonjwa wa kifua kikuu pia wanamaambukizi ya virusi vya ukimwi ambapo takwimu zinaonmyesha kuwa kifua kikuu na Ukimwi kwa pamoja huua watu 450,000 katika Afrika kwa kila Mwaka.
Athari  zake
Kama  kifua kikuu na ukimwi visipodhiobitiwa katika miaka 20 ijatyo zaidi ya watu Bilioni moja Duniani waambikizwa ugonjwa mmoja wapo na zaidio ya watu milioni 35 watakufa.

Anasema kuwa  mfanyakzi mgonjwa  huisababisha  kukatisha kwa mtiririko wa kazi na kupungua kwa uzalishaji kwa siku ,wiki,au miezi  ya kutokuwa kazini  na husababisha kuongezeka  kwa gharama kwa waajili kama vile ghalama za matibabu na gharama ya uelimishaji kwa kuwa vinashambulia lika la nguvu kazi.

Changamoto katika kukabiliana na ugonjwa huo
Mratibu huyo anasema kuwa   kuchangamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na Tiba za jadi kuingilia matibabu ya kifua kikuu,uelewa mdogo wa jamii kuhusu mahusiano ya kifua kikuu na ukimwi ikiwa ni pamona na  kutozingatia  masharti ya kitalaam katika matumizi ya dawa za kutibu kifua kikuu na ili kutunza ubora kwa wale wanaotumia dawa za kifua kikuu na Ukimwi.

Anazitaja  changamoto nyingine kuwa ni pamoja na Waratibu wa ugonjwa huo Wilayani  kupata usumbufu wa kutuma makohozi ya washikiwa wa kifua kikuu sugu kwenda maabara ya Taifa Muhimbili kwa njia ya posta wakati  kuna maabara ya kisasa iliyokamilika ya kupima vimelea hivyo katika maabara ya kifua kikuu katika hospitali ya rufaa Mbeya.

“Tatizo lillilopo katika maabara hiyo na kusababisha  Waratibu wa Wilaya kupata usumbufu huo ni kutokana  na  kukosa watalaam (Lab.Technologists)kwani maabara hiyo imejengwa  kwa fedha za Wahisani  Wamarekani hivyo hatuna Watalaam wa maabara”anasema

Changamoto nyingine ni kuwa ugonjwa huo kutopewa kipaumbele  katika mipango ya halmashauri na jamii na kuwepo kwa unayanyapaakwa watu waishio na kifua kikuu na ukimwi  na kutokuwa na lishe bora kwa wale waishjio na kifua kikuu na ukimwi.

Mwelekeo wa Mkoa kuhusu kudhibiti  ugonjwa huo
Dk Mwasubira anasema kuwa  kuweka mkakati maalum wa kuwafikia waganga wa jadi na jamii kwa ujumla ili kuinua kiwango cha uelewa,kuzihamasisha halmashauri za Wilaya kuongeza bajeti ya kudhibiti kifua kikuu katika mipango yao.

Anasema   mkakati mwingine ni kuwweka mkazo  wa upimaji wa kifua kikuu kwa kwenye virusi vya Ukimwi ,kuifanya maabara ya kifua kikuu sugu  hospitali ya rufaa Mbeya  kuweza kuchunguza  kifua kikuu sugu kwa kuotesha vimelea.
Mwelekeo mwingine ni kuwa na mkakati wa  kuimarisha uzuiaji wa maambukizi ya kifua kikuu katika sehemu  za kazi kwa watumishi wa afya na kushiriki katika tafiti za ndani na nje ya Mkoa.

Mwisho.

0 comments: