Kituo cha msaada wa kisheria
na unasihi Songwe (CHULECU) cha Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya,
kimeanza mpango wa kutafsiri sheria kwa lugha rahisi
kufuatana na mazingira husika, ili kuijengea uwezo jamii wa
kuzielewa sheria mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupunguza
migogoro ya ardhi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
kituo hicho Bwana Nyawili Kalenga, lengo la kuanzisha mpango huo ni kuiwezesha jamii kuzijua sheria mbali mbali
za nchi kwa kutumia lugha rahisi inayoeleweka katika jamii
husika.
Amesema kuwa kumekumekuwepo na
ukiukwaji wa sheria za nchi katika maeneo mbali mbali hasa vijijini, kutokana
na wananchi wa maeneo hayo kutozijua sheria, na baadhi ya watu kutumia uelewa wao mzuri wa sheria
kwa kuwanyanyasa wenzao ambao hawazijui na kujinufaisha kwa
masilahi yao binafsi.
Amesema kuwa mpango huo utawasaidia wananchi hasa wa
vijijini, ambao hawaijui lugha ya kiingereza na Kiswahili, kuzijua
sheria kwa kupitia lugha yao ambayo wanaitumia kwa wakati huo.
Amesema kuwa mfano sheria ya ardhi namba (4) na
(5) ya mwaka 1999, ambayo imeandikwa kwa lugha ya kiingereza, nimuhimu kwa Wananchi wa vijijini ambao mara nyingi imekuwa
ikitokea migogoro ya ardhi kwa wakulima na Wafugaji inayosababishwa na
ukiukwaji wa sheria hiyo.
Bwana Kalenga amefafanua kuwa endapo kama sheria hiyo
ikatafsiriwa kwa lugha rahisi kufuatana na mazingira husika ,
itawasaidia wakulima na wafugaji kujua haki zao na pia kuepuka
ukiukwaji wa sheria ikiwa ni pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi.
Mwisho
Brandy Nelson
0 comments:
Post a Comment