Pages

Thursday, November 14, 2013

WILAYA YA CHUNYA YATAKIWA KUGAWANYWA





 Uongozi wa Mkoa wa Mbeya na Wilaya ya Chunya umeagizwa kufanya mchakato wa kuangalia namna ya kuweza kuigawa wilaya hiyo ili kupata wilaya nyingine kwa lengo la kuwasogezea huduma jirani na wananchi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Hawa Ghasia, alitoa agizo hilo juzi  baada ya kutolewa mapendekezo na Madiwani wa Halamshauri ya Chunya hiyo ya kuigawa Wilaya hiyo kwenye kikao kilichowakutanisha watumishi wa idara mbalimbali wa Halmashauri hiyo.

Wilaya ya Chunya ina kilomita za mraba 29,219 sawa na asilimia 46  ya eneo zima la Mkoa wa Mbeya  lenye ukumbwa kilomita za mraba 63,617 huku idadi ya watu wake ikiwa ni  298,408.

Waziri Ghasia alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya hiyo ya Chunya ufanye mchakato huo haraka na kuwasilisha  vigezo vilivyopo Serikali kuu ili kuweza kuangalia vigezo hivyo kisha maamuzi ya kuigawa wilaya hiyo ufanyike.

“Anzeni mchakato wa kupata wilaya nyingine haraka na muulete kwetu, tunajua vigezo vinavyohitaji kupatikana wilaya mpya vinatakiwa viwe 10 lakini kwa Chunya ikizngatiwa na jiografia ilivyo hata vikifika sita tu tunaweza kufumba macho na kupitisha kwa vigevyo hivyo,” alisema Waziri Ghasia.

Alisema kuwa wilaya hiyo jiografia yake ni dhahirikwmaba kuna kila sababu ya  kupatikana kwa Wilaya nyingine ili kuwarhisishia wananchi kupata huduma kwa urahisi zaidi huku akibainisha kwa ni wilaa inayouidi hata Mikoa ya Kilimanjaro na Dar Es Salaam.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, agizo hil litafanyika haraka  iwezekavyo kwa kushirikiana na wataalamu mbaimbali wa Mkoai hapa katika kutafuta vigezo muhimu vinavyohitajika ili kuwapunguzia adha ya kusafiri mwendo mrefu wa wilaya hiyo kufuata huduma.

Awali madiwani wa Halmashauri hiyo, walisema kuwa kutokana na umbali wa kata na vijiji na miundombinu kuwa mibovu imekuwa tatizo kubwa katika kuwahudumia wananch jambalo linakwamisha
maendeleo.

Na Godfrey kahango

0 comments: