Pages

Wednesday, December 18, 2013

Mfanyabiashara wa kubadilisha fedha avamiwa na majambazi





MFANYABIASHARA ya kubadilisha fedha  katika mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya Alphonce Mwanjela(36)amevamiwa na kundi la watuwanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na kupigwa risasi mguu wa kuliana kuporwa  fedha  zaidi ya milioni 20 zikiwemo shilingi  zakitanzania, Dora za kimarekani,Randi ya Afrika Kusini na kwacha yaZambia.

Akizungumzia tukio hilo kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Barakael
Masaki alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana   majira ya saa 1:45
jioni juzi na  eneo la Sogea makambini Tunduma Wilayani Momba.


Alizitaja fedha hizo ambazo  majambazi hao walifanikiwa kupora kuwa ni
Shilingi za kitanzania milioni 5.2,Dora za kimarekani 2,300,Randi ya
Afrika kusini 10,000 na kwacha za Zambia milioni mbili.

Alisema kuwa  watuhumiwa hao walimvamia mfanyabiashara huyo akiwa
umbali wa mita 50 toka nyumbani kwake wakati anatoka katika shughuli
zake za kubadilisha fedha mpakani  Tunduma.

“Katika tukio hilo majambazi hao walianza kwa kumkata mapanga kichwani
na kumpiga risasi katika mguu wake wa kulia kwa kutumia  bunduki
idhaniwayo kuwa Short Gun na kumpora fedha hizo na kasha kutomea
kusikojulikana”alisema

Masaki alisema kuwa mfanyabiashara huyo amelazwa katika kituo cha afya
 cha Tunduma  na hali yake inaendelea vizuri na kwamba bado napatiwa
matibabu.

Aidha  Masaki  ametoa wito  kwa Wafanyabiashara ya kubadilisha fedha
wajiunge pamoja kwa ajili ya kufungua la kubadilisha fedha ambalo
litakuwa limesajiliwa  ili ulinzi uwe rahisi na kuondokana na suala la
kutembea na fedha kiholela  ili kuepusha matukio ya kuvamiwa na
majambazi kiurahisi.

0 comments: