MADIWANI
wanne kati ya 18 chama cha Demkrasia na maendeleo
Chadema na NCCR Mageuzi katika Jiji la Mbeya juzi walihojiwa na jeshi la polisi Mkoani hapa
kwa tuhuma za kughushi majina ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi na diwani wa Kata ya Forest Boyd Mwabulanga.
Juzi
Madiwani 18 wa chama cha Demkrasia na maendeleo Chadema na NCCR
Mageuzi katika Jiji la Mbeya walipata taarifa kwa njia ya simu kwa
ajili ya kuhojiwa na jeshi la polisi Mkoani hapa kwa tuhuma
za kughushi majina ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na diwani
wa Kata ya Forest Boyd Mwabulanga.
Kwa
mujibu wa Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Mbeya ambaye pia ni Diwani wa
Kata ya Mwakibete, Lucas Mwampiki madiwani waliohojiwa ni pamoja na
Uswege Furika diwani wa kata ya Ilemi, Deogratius Kapusi Diwani wa kata
ya mbalizi Road na madiwani wa viti maalum Esther Mpwiriza na Sarah Kitumbula
Mwampiki
alisema jana walipigiwa simu za kuitwa kuhojiwa na jeshi la polisi
ambapo madiwani 12 ndiyo waliofika katika ofisi ya RPC ambako ndiko mahojiano
hayo yalifanyika lakini kutokana na muda walkihojiwa madiwani wanne pekee.
“Kutokana
na muda walifanikiwa kuwahoji madiwani wanne na kutuambia sisi wengine
tuondoke watatuita siku nyingine kwa ajili ya kufanya mahojiano
hayo “alisema
Akizungumza
na Blog hii Diwani wa kata ya Forest ambaye pia ni kiongo
zi wa madiwani
wa upinzani katika halmashauri ya jiji la Mbeya Boyd Mwabulanga kuhusu
tuhuma za saini yake kugushiwa alisema kuwa yeye ndiy aliyeruhusu jina
lake liandikwe na kusainiwa kwani maamuzi hayo yalikuwa ya pamoja na siyo ya
madiwani wachache.
“Aliyepaswa
kulalamika kuwa saini yake imegushiwa ni mimi na siyo halmshauri au Mkurugenzi
hayo yalikuwa ni makubaliano ya sisdi madiwani wa upinzani na tulikubaliana
kuwa barua ya kuomba mkutano maalum iandikwe na mimi na mbunge tukabariki
majina yetu yaingizwa kwenye orodha hiyo sasa iweje walalamike wao kama
halmashauri”alihoji
Diwani
huyo ambaye yupo jijini dare s Salaam kwa ajili ya matibabu alisema kuwa
kitendo hicho cha kuwashitaki madiwani hao ni mbinu za baadhi ya viongozi
wa halmashauri ya jiji la Mbeya kutaka kuficha ukweli na kuzuia
hoja za madiwani wa upinzani kutojadiliwa katika kikao cha baraza la madiwani
kama kanuni zinavyoelekeza.
Hivi
karibuni baraza la madiwani liliazimia kuwachukulia hatua za kisheria madiwani
wa upinzani kwa tuhuma za kughushi sahihi za mbunge na diwani wakati wa
kuorodhesha majina ya madiwani waliotaka kuitishwa kwa kikao cha dharura wa
kujadili kutofuatwa kwa ratiba ya vikao vya halmashauri na kuhitaji ufafanuzi
wa matumizi mabaya ya Shilingi milioni 95 zinazodaiwa kutumiwa na maofisa
watano wa jiji walipotembelea nchini China,
0 comments:
Post a Comment