Washiriki na mafunzo ya haki za afya ya uzazi kwa vijana wakifanya kazi za vikundi yaliyoandaliwa na shirika la AMREF na kufanyika katika chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA)Morogoro
Imeelezwa
kuwa wazazi na familia za
Kiafrika hawana utaratibu wa kutoa elimu ya afya kwa watoto wao walio na
umri kuanzia miaka 10 hadi 16 kwa madai
kuwa watakuwa wamechangia watoto hao kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi.
Hayo yamebainika katika kituo cha watu wanaoishi na
virusi vya Ukimwi Morogoro(WAVUMO)waliokuwa wakizungumza na waandishi wa habari
waliopo katika mafunzo ya haki za afya
ya uzazi kwa vijana yaliyoandaliwa na shirika la utafiti wa madawa na Tiba
(AMREF) walipotembelea kituo hicho.
Akizungumzia tatizo hilo muuguzi wa kituo hicho
Monica Kayembele alisema kuwa tamaduni na mira za kiafrika wazazi wengi hawana
utamaduni wa kutoa elimu ya uzazi kwa watoto wao kwa imani kuwa watakuwa
wanashiriki kuchangia watoto wao kujiingiza katika mahusiano ya kiimapenzi.
Alisema kuwa mara kadhaa kituo hicho kimekuwa kikipokea watoto ambao
wamekuwa wakiletwa na wazazi wao kwa malengo ya kupewa elimu kuhusu maambukizi
ya virusi vya ukimwi kutokana na kuambukizwa na wazazi wao.
“Kutokana
mila wazazi wengi kuongelea masuala ya uzazi wamekuwa hawapo wazi hivyo
kusababisha masuala ya maambukizi na mimba za utotoni kuendelea kujitokeza”alisema
Kwa upande wake mratibu wa kituo hicho Sara Mokiwa
alisema kuwa kituo hicho pia kimekuwa kikipokea watoto ambao walipata maambukizi kutokana na vitendo vya ubakaji
na wengine kwa kujiingiza katika masuala ngono wakiwa katika umri mdogo.
Aidha alisema kuwa kituo hicho kinahudumia watu 3267
wakiwepo watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 14 idadi yao 156,umri kati ya 15 hadi 17 watoto
27 na unri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea wakiwa 3081.
Kwa upande wake mama mmoja aliyejitambulisha kwa
jina la Sikujua John mkazi wa kikundi
alisema kuwa mila na tamaduni zilizozoeleka tangu enzi za mababu ni
mwiko kwa mzazi kumweleza mtoto ambaye bado ahajakua masuala ya afya ya uzazi.
“Unajua waandishi kitu hiki nikigumu na hakiwezekani
kwani hata sisi wakati tunakua wazazi wetu walikuwa wakitudanganya kuwa
wananunua watoto dukani na siyo kwamba mama amejifungua mtoto na ndivyo
tulivyoa amini kuwa watoto wananunuliwa dukani “alisema
Naye mtoto Joseph Januari mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa
mtaa wa uhuru alipohojiwa kama amewahi kupata taarifa yoyote kuhusu afya
ya uzazi alisema kuwa hajawahi kusikia zaidi ya kusikiliza matangazo ya television
na radio.
0 comments:
Post a Comment