Shirika la
utafiti wa madawa na tiba (AMREF) limetoa
mafunzo ya haki za afya ya uzazi kwa vijana kwa baadhi ya Waandishi
wa habari na Wahariri nchini ili kuwajengea uwezo wa kuandika kwa undani habari za afya ya uzazi na kuibua changamoto
zake katika jamii .
Mafunzo hayo
ya siku tatu yanafanyika katika chuo cha
kilimo SUA na kushirikisha waandishi 22 kutoka katika mikoa ya Njombe,Iringa,Mbeya,Morogoro
na dar es Salaam
ambapo pia waraweza kujifunza uandishi wa
habari za kiuchunguzi na maadili ya uandishi wa habari za afya ya uzazi
kwa vijana.
Kwa mujibu
wa mchambuzi wa sera na mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka AMREF Meshack Mollel malengo ya mafunzo hayo kuwezesha waandishi kuwa na
uwelewa kuhusu afya ya uzazi kwa vijana
na kuweza kuandika kwa undani habari za afya ya uzazi kwa vijana.
Mollel alisema kuwa AMREF inatekeleza mradi wa
haki za afya ya uzazi kwa vijana katika
kipindi cha miaka mitatu kwa Wilaya tatu za Ilala na Kinondoni kwa mkoa wa Dar es Salaam na Manspaa ya
Iringa.
“Kutokana na
kuwepo kwa mradi shirika likaona ni vema likatambua umhimu wa waandishi wa
habari kupata mafunzo haya na kuweza
kushirikiana na shirika katika kuandika habari kwa undani za afya ya uzazi kwa
vijana na kwenda vijijini kubua changamoto
kwa jamii”alisema
Alisema kuwa
katika mradi AMREF imelenga kuwafikia 100,000 katika kipindi cha miaka mitatu
kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 na kwa vijana 100 wenye ulemavu wa kusikia wenye
umri wa kuanzia miaka 10 hadi 24.
Mollel
alisema kuwa katika mradi huo tayari vituo viwili vimeanzishwa kwa ajili ya
vijana kwa ajili ya kutoa afya ya uzazi kwa vijana ambapo vijana wanapata nafasi ya kuelimishwa
na kupata tiba ya afya ya uzazi na kwamba kuna maeneo makuu ya mradi ambayo ni pamoja na huduma rafiki za
afya ya uzazi kwa vijana,utetezi na sera ya afya ya uzazi kwa vijana na kujenga
uwezo kwa watoa huduma.
0 comments:
Post a Comment