Mchambuzi wa Sera kutoka shirika la utafiti wa dawa na tiba (AMREF)Meshack Mollel akitoa mada juu ya uandishi wa habri za afya ua uzazi kwa vijana kwa Waandishi wa habari na Wahariri kutoka mikoa ya Iringa,Njombe,Mbeya,Morogoro na Dar es Salaam katika chuo cha Kilimo SUA Morogoro.
Imeelezwa kuwa hakuna mfumo maalum wa upatikanaji wa taarifa za afya ya uzazi kwa
vijana na kuwasababishia kupata
changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi,mimba
za utotoni na magonjwa ya zinaa.
Hayo
yameelezwa na mchambuzi wa sera katika shirika la utafiti wa madawa na tiba (AMREF)Meshack Mollel alipokuwa akizungumza katika semina ya siku
tatu ilitolewa na shirika hilo kwa waandishi wa habari kuhusu haki za afya ya uzazi kwa vijana inayofanyika
katika chuo cha kilimo SUA Mkoani Morogoro.
Alisema kuwa ni muhimu kwa vijana kuanzia umri wa miaka 10
hadi 24 kupata taarifa za uzazi ili
kuweza kukabiliana na changamoto zinazowazunguka katika mazingira yao na kwamba
idadi kubwa vijana ndiyo wanaoathiriwa na changamoto
hizo.
“Kwa mujibu wa Sensa ya watu ya hivi karibuni
idadi kubwa ya Watanzania ni vijana hivyo jamii inapaswa kutambua kuwa
hawa vijana wanahaki ya kupata afya ya uzazi ili kuwaepusha katika matatizo
ambayo tumekuwa tukiyashuhudia katika maeneo yetu yanayozunguka”alisema
Mollel
alisema kuwa kati ya wakina mama 8000
wanaokufa kila mwaka kutokana na uzazi asilimia kubwa ya
wakina mama hao ni vijana na kwamba vijana wanachangia katika maambukizi ya mapya
ya virusi vya ukimwi kwa asimilia 60.
Alisema
kuwa kuna haja kwa serikali kuona
umuhimu wa uwepo wa vituo vya kutolea tarifa ya afya ya uzazi kwa vijana ili
kuweza kukiokoa kizazi cha vijana ambacho
ndiyo nguvu kazi kubwa tegemeo kwa Taifa
ambacho kwa sasa kimekuwa kikiathirika kutokana na kukosa haki ya kupata
taarifa afya ya uzazi.
Aidha alisema kuwa
wakati sasa umefika kwa jamii kuondokana na mila potofu za kuzuia watoto
kupata elimu za afya ya uzazi kwa madai
ya kuwa na umri mdogo huku kukiwa na matukio mengi ya mimba za utotoni.
0 comments:
Post a Comment