Wakati shule za msingi nchini
zimefunguliwa baada ya mapumziko yamhula wa kwanza,shule mbili za msingi za
Mapambano na Nero katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya hazina huduma za vyoo
tangu mwaka 2012.Imeelezwa
Shule hizo za msingi ambazo zina wanafunzi zaidi ya
2600,huduma ya vyoo imekosekana kutokana na matundu ya vyoo takribani 32
yamejaa,hali inayoweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kwa wanafunzi hao.
Wakizungumza na Mwandishi wa habari
hizi Wanafunzi wa shule hizo ambazo zipo jirani
walisema kuwa ni kwa muda mrefu shule hizo vyoo hivyo vimejaa na
kusababisha kujisaidia maeneo ambayo
siyo husika kama kwenye maeneo ya viwanja ya shule hizo.
“Hali ni mbaya ya vyoo vyetu
kwani hili tatizo ni la muda mrefu na
hasa kwa sisi watoto wa kike tunapata shida mara tunapohitaji kujisaidia wakati
mwingine inatulazimu kwenda kwenye nyumba za jirani kuomba msaada hali ambayo
pia inatufanya kuona mazingira magumu “alisema
Marietha Yohana mwanafunzi wa shule ya msingi Nero
Naye Mwanafunzi wa
shule ya msingi Mapambano Andrew Mwaigomole alisema kuwa mazingira ya vyoo vya shule hiyo ni mabaya
hayafai kwa afya ya binadamu kwani
rahisi kupata magonjwa ya mripuko hivyo
hatua za haraka zinahitajika
katika kutatua tatizo hilo.
Akizungumzia tatizo hilo Mwalimu Mkuu
wa shule ya msingi Nero Gasper Lyimo
alisema kuwa kamati ya shule na serikali
ya mtaa inataarifa ya tatizo hilo na
kwamba shule yake ina matundu 17 ya vyoo ambapo
yote yamejaa na kuziba.
“Watoto wanajisaidia kwa kuzibua kidogo matundu hayo hali ambayo ni hatari kwa afya
zao lakini tulitoa taarifa kwa kamati ya shule ambapo walikubaliana na wazazi
kuchangia ujenzi wa vyoo hivyo”alisema
Mwenyekiti wa
kamati ya shule ya
Nero Joyce Mwaituka alisema kuwa
jukumu la ujenzi wa vyoo katika
shule za msingi ni la Wazazi ,uongozi wa
mitaa miwili ya kata ya Iyela ndiyo
weneyejukumu la kuhudumia shule zao
“Baada ya kupata taarifa tulikubaliana kila mzazi achangiae Sh4,000 na kuna zaidi ya wazazi 3,000 kwa shule zote lakini ni Wazazi 80 pekee ndiyo waliochangia
fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo “alisema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Serikali ya mtaa wa Iyela two Ezekiel Mwakilasa alikiri kuwepo kwa changamoto
hiyo na kwamba mara nyingi wamekiwa wakijadili kwenye vijao na kwamba gharama
ya ujenzi wa vyoo hivyo ni Sh38 milioni ambapo hadi sasa imepatikana Sh1.6 milioni.
Aidha baadhi ya wazazi wa kata ya Iyela wametupia lawama kwa viongozi wa kata ya Iyela kwamba
wametanguliza siasa mbele ambapo baadhi yao wamekuwa wakiwashawishi wazazi
kuchangia kiwango cha Sh2,000 badala ya Sh4,000
waliyokubaliana na kusababisha kukwama kwa ujenzi wa vyoo hivyo.
0 comments:
Post a Comment