KANISA la
Moravian jimbo la Kusini Magharibi
limeingia katika mgogoro mkubwa
baada ya bodi ya kanisa hilo kumsimamisha
kazi
Mwenyekiti wake Mchungaji Nosigwe Buya na kudaiwa kubadilisha vitasa vya mlango wa
ofisi yake huku mwenyekiti huyo akikaidi
kusimamishwa kwake na kuahidi kuendelea
kutoa huduma kwa waumini .
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti huyo Mchungaji Nosigwe Buya kuhusu kusimamishwa kwake
alisema kuwa hakubaliani na hatua hiyo kwani barua aliyokabidhiwa ya
kusimamishwa kwake haikujitosheleza kutokana
na kutoonyesha sababu za kusimamishwa.
“Ni kweli nimekabidhiwa barua
ya kusimamishwa kwangu ya tarehe Januari 03,2014 ambayo imeeleza kuwa nimesimamishwa kazi ya
Uwenyekiti hadi mwaka 2016 katika mkutano wa sinodi ya uchaguzi
kwa makosa 11 na Bodi ya Kanisa itanipangia kituo kingine cha kazi”
“ Kutokana na barua hiyo sijatendewa haki kwani hadi sasa
sijui makosa yangu kwani awali nilikubali kusimamishwa katika kipindi cha
miezi mitatu kuanzia Julai,31 hadi Oktoba kwa lengo la kuipisha tume kufanya
uchunguzi juu ya matumizi ya fedha Sh200 milioni za mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya
Mbozi “alisema
Alisema kuwa baada ya bodi kumsimamisha katika kipindi hicho
cha miezi mitatu aliongozewa miezi mingine
miwili na ndipo ilipofika Januari 03,2014 alikabidhiwa barua ya kusimamishwa hadi mwaka 2016 wakati
wa sinodi ya uchaguzi.
Mwenyekiti huyo ambaye
pia ni Mwenyekiti wa makanisa ya
Moravian Afrika alisema kuwa hadi sasa uongozi wa kanisa hilo haujatoa ripoti
ya tume kwa waumini na wachungaji na kwake
na badala yake umechukua uwamuzi wa kumsimamisha bila kuelezwa sababu 11 zilizotajwa katika
barua hiyo.
“Msimamo wangu kwa sasa mimi bado ni Mwenyekiti na
nitaendelea kuhudumia waumini wangu pamoja na kuwa tayari ofisi yangu
wamebadilisha kitasa na kuu funga na nimeandika barua ya kuitisha mkutano wa Sinodi ya dharula ambapo wajumbe
wake ni Wachungaji na mjumbe mmoja mkristo kutoka kwenye ushirika ambayo itafanyika January 18,2014 katika kanisa la Bethrehem eneo la mama
John”alisema
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa makanisa ya Moravian Afrika alisema kuwa
lengo la kuhitisha Sinodi hiyo ni kuwataka waumini na Wachungaji kupata
ukweli na kama kuna makosa”nipo tayari
kujihudhuru na kuacha nafasi yangu
ichukuliwe na mtu mwingine”alisema
Wakizungumzia mgogoro huo baadhi ya wachungaji ambao
hawakutaka majina yao kutajwa gazetini walisema kuwa kilichofanyika katika
jimbo hilo ni kutaka kuleta mpasuko ndani ya kanisa kwani hata barua
walizokabidhiwa kuhusu kusimamishwa kwa Mwenyekiti hazijaeleza sababu ya
kusimamishwa kwake.
“Kama wachungaji tunasikitishwa na hatua ya jambo hili
ilipofikia na kwa sasa tunashuhudia wazi kuwepo kwa mpasuko mkubwa ndani ya
kanisa kwani nasi hatutakubaliana ni hii
hali kama mwenyekiti amebainika kuwa na makosa ni vema tukajulishwa ili tuweze
kufahamu kama kuna halali kusimamishwa au kaonewa kama anavyodai
yeye”alisema mmoja wa Wachungaji hao
Katibu Mkuu wa
jimbo hilo Willey Mwasile alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alikiri
kuwepo na kwamba kwa sasa msemaji wa jimbo hilo ni Makamu Mwenyekiti
Mchungaji Zakaria Sichone “hivyo
nakushauri ukamuone ndiye anaweza kutoa maelezo hayo yote “alisema
Kwa upande wake Makamu mweyekiti wa jimbo hilo Mchungaji
Zakaria Sichone alipotakiwa kueleza sababu za kumsimamisha Mwenyekiti
huyo alisema kuwa hilo jambo linahusu mambo
ya kiroho na kumtaka mwandishi kusubiri hadi hapo kikao cha halmashauri
kuu kinachotarajjia kufanyika siku ya ijumaa kwa ajili ya suala hilo.
“Ni kweli waumini
wanahaki ya kufahamu ukweli kuhusuana na jambo hili lakini pia Mwenyekiti amekiuka taratibu kwa
kuamua kuingia ofisini na kuendelea na kazi wakati tayari alikuwa
ameshasimamishwa tangia awali na yeye
kukabidhi ofisi hivyo nakuomba
ndugu mwandishi nitakutafuta kwa
ajili ya kukueleza hili suala mara baada ya bodi na halmashauri kuu kukutana”alisema
0 comments:
Post a Comment