BAADA ya kusuasua
na kuzua hofu kubwa kwa wadau wa soka mkoani Mbeya,Hatimaye kazi ya kupanda
nyasi ndani ya uwanja wa Sokoine imekamilika kwa asilimia 95, tayari kwa
michezo ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Akizungumza katika mkutano
wa waandishi wa habari jana , Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Mbeya
(Mrefa), Elius Mwanjala, zoezi hilo limeghari kiasi cha shilingi milioni 22.3
hadi kukamilika kwake.
Hata hivyo, Mwanjala aliwataka
wadau wa soka kujitokeza ili kusaidia kiasi cha shilingi milioni 4 ili ziweze
kusaidi kazi iliyobaki ya asilimia tano, kwa kuwa chama hicho
kimeishiwa na hakina uwezo wa kupata fedha hizo kwa haraka.
Aidha, amewatoa hofu
wadau wa soka na kusema asilimia tano iliyobaki haiwezi kuasili ratiba ya mechi
za mzunguko wa kwanza na kwamba michezo yote ya mzunguko wa pili iliyokuwa
ichezwe ndani ya uwanja huo itafanyika bila kikwazo chochote.
Alisema kama fedha hizo
kiasi cha shilingi milioni 4 zikipatikana kwa muda muafaka uwanja huo unaweza kukamilika
kwa asilimia 100 ndani ya wiki ijayo hivyo kutoa mwanya mechi za mzunguko wa
pili kuchezewa ndani ya uwanja huo mkongwe wa Sokoine.
Mwanjala alisema kuwa pamoja na kufikia hatua hiyo bado kuna changamoto
inayowakabili ikiwa ni pamoja na deni la
kiasi cha shilingi milioni 13.8
lililotokana na wadau kukikopesha fedha
hizo chama hicho kwa ajili ya
ujenzi wa uwanja huo.
Aidha aliwashukuru wadau wote waliojitokeza kusaidia
kwa hali na mali zoezi zima, lakini shukurani kubwa amezielekeza kwa Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya kuamua kuamua kusaidia nguvu kwa kutoa askari wa jershi la
kujenga taifa (JKT).
Akifafanua zaidi,
Mwanjala alisema kitendo cha JKT kuongeza nguvu kimechangia kwa kiasi kikubwa
kukamilika kwa wakati kwa upandaji nyasi ndani ya uwanja huo.
Uwanja wa Sokoine Mbeya unatumiwa na
timu mbili za ligi kuu ya Vodacom, ambazo ni Mbeya City inayofanya vizuri ,
pamoja na Tanzania Prisons,
0 comments:
Post a Comment