Mwenyekiti wa chama cha
Mpira Mkoa wa Mbeya (MREFA)Elias Mwanjala
amesema kuwa uwanja wa kumbukumbu ya
sokoine umekuwa ni uwanja wa pili
kimapato ukiongozwa na uwanja wa Taifa kutokana na kuwepo kwa timu ya Mbeya
City.
Mwanjala alisema
kuwa kutokana na kuwepo kwa timu ya
Mbeya City kumeongeza idadi kubwa ya mashabiki ambao wamekuwa wakiingia katika
uwanja huo mara timu hiyo inapokuwa inacheza kuwezesha kuingiza fedha nyingi
ambazo hazikuwahi kutokea huko nyuma.
“Katika hili lazima tuseme
wazi kuwa uwan ja huu wa Sokoine umekuwa pili kimapato ukiongozwa na na ule wa Taifa sababu ya kuwepo kwa mbeya
City kwani timu hii imekuwa na mashabiki ambao wakuwa wakijaa uwanjani mara
timu hii inakuwa na mechi”alisema
Alisema kuwa mashabiki
hao wa Mbeya City pia wamekuwa wakijitolea kwenda kushuhudia mechi za nje za timu yao kama vile
jijini Dar mechi ya Simba na Azam na Tanga ambapo pia waliweza kuongeza mapato
katika michezo hiyo.
“Awali uwanja wa sokoine
ulikuwa ukipata mapato makubwa wakati wa
mechi za Simba na Yanga zinapokuja kucheza hapa lakini hata hivyo ujazaji wa
mashabiki hauwezi kuifikia timu ya Mbeya City ilipokutana na timu ya Yanga na
nyinginezo katika mzunguko wa kwanza
ligi kuu ya Vodacom”alisema
Alitoa mfano wa mechi kati ya timu Yanga Afrikan na Mbeya City iliyofanyika ambapo
timu hizo zilitoka sare ya 1-1 iliingiza wato 20,000 na mapato yalikuwa ni
Sh100 milioni katika uwanja wa
kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa.
0 comments:
Post a Comment