Naibu Waziri wa afya na ustawi wa jamii DK Seif Rashid akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa vya Tiba kwa Mikoa ya Tanga na Mbeya katika ukumbi Hospitali ya Mkoa wa Mbeya |
Naibu Waziri
wa afya na ustawi wa jamii Dk Seif Rashid jana amekabidhi vifaa tiba
kwa mikoa ya Tanga na Mbeya vyenye thamani
ya Sh989.1 milioni kwa ajili ya mradi wa mama na motto
unaotekelezwa kwa ushirikiano na mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHFI) na
benki ya maendeleo ya watu wa Ujerumani(KfW).
Akizungumza
kabla ya kukabidhi vifaa hivyo naibu Waziri huyo alisema kuwa serikali
inatambua umuhimu na kuenzi jitihada zinazolernga kuboresha afya ya mama na
mtoto kwani hakuna haja ya mama mjazito kupoteza maisha wakati wa kuleta kiumbe hai.
“Kutolewa
kwa vifaa hivyo ni ishara ya kuwa tunaweza kuboresha huduma za akina mama
wajawazito na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ikiwa tutashirikiana
kukusanya nguvu za pamoja na kuliona suala hili kuwa ni wajibu wa kila
mmoja”alisema
Alisema
kuwa kupunguza idadi ya vifo vya wakina
mama wajawazito inawezekana kwani
takwimu zinaonyesha kuwa nchi ya Uingireza kuna vifo sita kati ya wakina
mama wajawazito 100,000 kwa mwaka na wa
Tanzania ni vifo 454 kati ya wakinamama 100,000 huku mikoa ya
Iringa na Mbeya ikiwa na vifo chini ya 200 kati ya wakina mama 100,000 kwa kila
mwaka.
Aidha ameziagiza
halmashauri zote za mkoa wa Tanga na Mbeya kuhakikisha baada ya miezi sita
kuanzia sasa ziwe zimewasilisha madai ya fedha za tele kwa tele na kuzipata fedha hizo ili kuweza
kuboresha huduma ya afya.
Awali akitoa
taarifa ya mradi huo Kaimu Mkurugenzi
mkuu wa NHFI Hamisi Mdee alisema
kuwa katika mradi huo jumla ya walengwa
74,099 wameshafikiwa ambao ni sawa na asilimia 105 kati ya lengo la kuwafikia
akina mama wajawazito 70,000 kufikia Desemba 2014.
Alisema kuwa
kupitia mradi huo kiasi cha Sh644.1milioni zimelipwa kwa vituo vya matibabu vya
mikoa ya Tanga na Mbeya vilivyotoa huduma
kwa akina mama wajawazito na Sh400.4 zimetumika kulipia familia za akina
mama hao ili kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (chf) na hivyo kuziwezesha halmshauri 12 za mikoa
ya Mbeya na Tanga kuomba fedha za tewle kwa tele kutoka NHFI.
Mdee alisema
kuwa katika utekeleza wa mradi huu kuna changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja
na vituo vya huduma kutowasilisha madai yao kwa huduma walizotoa kwa akina mama
wajawazito pamoja na kuwa wamekuwa wakilipwa na NHFI na wananchi kutofikiwa na elimu kuhusu huduma za usalam na
huduma za mifuko hiyo miwili.
0 comments:
Post a Comment