Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi mwanadmizi wa polisi Ahmed Msangi. |
Watu wawili wameuawa katika
matukio tofauti Mkoani Mbeya akiwemo mkazi wa kijiji cha Kapele Wilaya ya Momba aliuawa kwa kuchomwa kisu
mgongoni na mdogo wake kwa madai ya kulipiza kisasi baada ya kutangaza
mtuhumiwa kuwa alitorosha mke wa mtu.
Kamanda wa polisi Mkoa wa
Mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi amewataja waliouawa kuwa ni pamoja na
Adam Silumbe (27) mkazi wa kijiji cha Kapele
Wilaya ya Momba na Bicco Mwakabibi (28)
mkazi wa kijiji cha Lema Wilaya yha Kyela.
Akizungumzia matukio hayo Msangi alisema kuwa tukio la mauaji ya Adam Silumbe lilitokea Junuari 10mwaka huu majira ya saa 3:000 usiku
baada ya marehemu kuchomwa kisu mgongoni
na mdogo wake Bonny Silumbe katika
kijiji cha Kapele Wilaya ya Momba.
Alisema kuwa baada ya
kufanyika kwa tukio hilo marehemu alikimbizwa katika hospitali ya serikali Wilaya ya Mbozi ambapo alifariki jana majira
ya Saa 3:30 asubuhi alipokuwa akiendelea
kupatiwa matibabu.
Kamanda Msangi alisema kuwa
chanzo cha tukio hilo na mtuhumiwa alitoroka mara baada ya kufanya tukio hilo
na kwamba mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa
kwa familia yake kwa ajili ya mazishi.
Katika tukio lingine marehemu
Bicco Mwakibibi aliuawa kwa kupigwa
sehemu mbali mbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua
kujichukulia sheria mkononi wakitumia silaha za jadi mawe na fimbo kwa tuhuma za wizi kayika
kijiji cha Lema Wilaya ya Kyela.
Kamanda Msangi alisema
kuwa marehemu na mwenzake wanatuhumiwa
kuvunja kibanda cha biashara na kuiba na kwamba baada ya tukio wenzake alikimbia na kwamba juhudi za kumtafuta
zinafanyika.
0 comments:
Post a Comment