Wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi Wilaya ya Mbeya wakiangalia gari aina ya Coaster mara baada ya kogongana na roli eneo la Mlima Mbalizi Wilaya ya Mbeya.
WATU wawili wakufa papo hapo jana na
wengine 23 kujeruhiwa, baada ya basi aina ya Coaster waliyokuwa wakisafiria
kutoka Jijini Mbeya kuelekea Tunduma kugongwa kwa nyuma na Lori la mizigo
katika eneo la mlima Mbalizi Wilaya ya Mbeya vijijjin.
Aidha katika katika hali isiyokuwa ya kawaida askari wa
kutuliza ghasia waliofika muda mfupi baada ya kutokea ajali hiyo walilazimika
kufyatua lisasi hewani ili kuwatawanya watu walionza kupora vitu baada ya Lori
hilo kuanguka lilimwaga bidhaa
mbalimbali za madukani, zikiwemo sabuni hali iliyofanya wananchi kuanza kuvamia
kwa lengo la kupora.
Akizumgumzia ajali hiyo mmoja wa shuhuda John Mwakambo alisema kuwa ilitokea jana majira ya saa 10:45, wakati
magari hayo yakitelemka katika mtelemko mkali wa mlima Iwambi ,karibu na mji
mdogo wa Mbalizi.
“ Lori hilo la mizigo lenye namba za
T 101 CLR na Tela lake T 859 BZW aina ya Scania liliigonga Coaster hiyo yenye
namba T 910 BFB kwa nyuma kwani lilionyesha kama kulikuwepo na tatizo la
kuharibika mfumo wa breki”alisema
Akifafanua zaidi shuhuda huyo,
alisema wakati Lori hilo likishuka kwa kasi mbele kulikuwa na gari nyingine
aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 370 AST lililokuwa likipandisha
hivyo kumchanganya dereva wa Lori hilo hivyo kuligonga kwa nyuma basi hilo la
abiria.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa
Mbeya, Barakaeli Masaki alithibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kusema watu
wawili walifia papo hapo ambao hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika mara
moja.
Alisema kuwa kuwa kati ya majeruhi hao 23, majeruhi 17
walipelekwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya na wengine sita walikimbizwa katika
Hospitali teule ya Ifisi iliyoko wilaya ya Mbeya Vijijini
0 comments:
Post a Comment