Wakulima katika kata ya Harungu Wilaya ya Mbozi Mkoani
Mbeya wamesema kuwa kuwepo kwa soko huria kumechangia mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani
kutotekelezwa na kusababisha maghala kutotumika kwa muda mrefu na kuua vyama
vya ushirika.
Akizungumza
kwa niaba ya Wakulima hao mbele ya Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro mara baada ya kutembelea kata hiyo mjumbe wa bodi
ya chama cha msingi cha ushirika
kata ya Harungu Andrew
Nyingi alisema kuwa Wakulima wamekuwa wakiuza mazao yao yakiwa
bado shambani kwa bei ndogo .
Alisema kuwa
kwa upande wa zao la kahawa wachuuzi wamekuwa wakiwashinikiza wakulima kununua
kahawa mbichi ikiwa bado shambani huku
maghala yaliyojengwa kwa malengo ya kutumia mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani
yakikaa bila kutumika kwa muda mrefu.
“Haya
maghala kwa sasa ni mabovu na hayajatumika kwa muda mrefu na kutokana
na kuwepo kwa soko huria na mazao yetu kukosa soko la uhakika kwani wanunuzi
wamekuwa wakinunua mazao yetu shambani bila kuwepo kwa utaratibu “alisema
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Dk. Charles
Mkombacheka alisema kuwa
kuna jumla ya maghala 54 yaliyojengwa kwa nguvu za Wananchi miaka ya 80 katika
Wilaya hiyo lakini hayatumiki, na kwamba kati ya hayo 28 yanatarajiwa kuanza kufanyiwa ukarabati ambao unakadiliwa kugharimu Sh 1.4 bilioni .
Kwa upande
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alisema kuwa
ni lazima ushirika urudishwe na
kuimalisha vikundi vidogo vya
wakulima na kuyafufua maghala hayo kwa kuendeleza mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani
ili kumsaidia mkulima kupata soko la uhakika wa mazao yao na kuondokana na
umasikini.
Aidha
kandoro alisema kuwa ni lazima wakulima
kuwa na uelewa wa mfumo huo wa
stakabadhi ya mazao ghalani hivyo Serikali
inawajibu wa kuhakikisha elimu hiyo inatolewa ili kuweza kumsaidia mkulima katika shughuli nzima ya
kilimo chenye manufaa.
“Mfumo huu
stakabadhi ya mazao maghalani unamlinda mkulima hivyo
hatunabudi kuhakikisha wakulima
wanapatiwa elimu kwanza na ndipo tuanze kuutekeleza mfumo huu na kurudisha vyama vya ushirika ambavyo ndiyo
msimamizi wa mkulima katika upatikanaji
wa soko la uhakika la mazao yao”alisema
0 comments:
Post a Comment