Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa katika moja ya miradi ya maendeleo katika kijiji cha Mshewe halmshauri ya Wilaya ya Mbeya |
Kandoro
alibaini hayo juzi alipotembelea kijiji hicho ambapo kuna ujenzi wa mradi wa mfereji wa maji kwa ajili ya kilimo cha
umwagiliaji ulioibuliwa na wananchi unaotarajia kugharimu kiasi cha Sh 208 milioni
hadi kukamilika kwake.
Akitoa
maelezo ya mradi huo Diwani wa kata ya Inyala Kisemba Mwalingo alisema kuwa awali kulikuwa na kikundi kilichodai
kuwa kinatoka katika kijiji hicho ambacho
kiliwasilisha andiko la kuomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo na kupewa kiasi cha Sh108 milioni.
Alisema kuwa
baada ya fedha hizo kuingia kwenye akunti ya kikundi hicho wahusika walianza
kutumia fedha hizo ambpo awamu ya kwanza
walichukua Sh10milioni na awamu ya pili walichukua Sh 11milioni huku mkandarasi akiwa hajatafutwa.
“Mara baada
ya kuchukuliwa fedha hizo ndipo ilipobainika kuwa kikundi hicho
siyo halali na hakitambuliki hapa kijijini kutokana na wananchi kueleza kuwa watu hao
siyo wenyeji katika kijiji hicho”alisema
Alisema
kuwa baada ya kufuatilia na kufanya uchunguzi wa kina ilibainika kuwa
kikundi hicho ni cha mtu mmoja na ndipo
Mkurugenzi alipochukua hatua za kuzuia akunti hiyo isitoe fedha zingine “wakati
tayari walikuwa wameshatoa fedha jumla ya Sh21milioni”alisema
Kwa upande
wake Kandoro alimwagiza kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kumfikishia wale wote waliohusika utoaji wa
fedha hizo ikiwa ni pamoja na kuwataka
kurudisha fedha hizo za seerikali ambazo zililetwa kwa ajili ya maendeleo ya
Wananchi.
0 comments:
Post a Comment