Pages

Thursday, February 6, 2014

Wafanyabiashara Tunduma waishangaa serikali

Naibu Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akiwa mpaka wa Tanzania na Zambia Tunduma Wilaya ya Momba akikagua mpaka huo hivi karibuni
Wafanyabiashara  wa mamlaka ya mji mdogo Tunduma Wilaya ya Momba mkoani Mbeya wameishangaa serikali kushindwa kumdhamini  mfanyabiashara ambaye ni mwekezaji wa ndani atakayeweza kutengeneza ajira na badala yake anadhaminiwa mbunge atakayedumu madarakani kwa miaka mitano.

 
Waliyasema hayo jana mbele ya  Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba katika risala yao iliyosomwa na Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara,viwanda na kilimo(TCCIA) Wilaya ya Momba Simon Kitojo  kwenye m kutano uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya High Class Tunduma.

“Tunashangaa tunaposikia mwanasiasa husudani Mbunge ndani ya miaka mitano ya kuchaguliwa kwake  serikali inamdhamini mkopo bila dhamana yoyote wa zaidi ya Sh300milioni laki ni serikali hiyo hiyo inashindwa kumdhamini mfanyabiashara ambaye atawekeza  ndani ya nchi kwa muda mrefu zaidi na kuongeza ajira ambayo ndiyo atitizo na kilio cha serikali yetu cha watu kukosa ajira”alisema Mwenyekiti huyo

Kitojo alisema kuwa Serikali kimekuwa kiimba wimbo  wa kutaka kuona Tanzania ina kuwa ni nchi ya viwanda kwa maana ya kuimarisha sekta ya kilimo na uongezaji wa thamani ya mazao.

”Kwa wimbo huu hatuoni kama inasema kweli na sisi tunaona kama inaongelea zaidi wawekezaji wa nje kuliko  wa ndani kwa vile wa tanzania wengi hasa wafanyabiashara wanajulikana nguvu yao na dhamana zao hivyo hawawezi kuwekeza kwa kiwango kinachotakiwa bila ya serikali kusimama kama dhamana ya mkopaji kwa kuywa dhama zetu ni za mikopo ya kujikimu tu na sio kuanzisha miradi mikubwa”alisema

Aidha  alisema kuwa kuna changamoto za kimfumo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya biashara ambpo toka serikalik ilipojitoa kwenye uchumi hodhi na sekta binafsi kuendesha uchumi huku serikali ikikusanya kodi pekee hakujawa na elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla wake juu ya kuwaelimisha wafanyabiashara kufanya biashara kwa ufanisi zaidi.

“Tunaiomba  serikali ishirikiane na sekta binafsi kuendesha mafunzo nchi nzima kwa wafanyabiashara kwa lengo la kujua haki zao,kujitambua,kujua wajibu wake kwa Taifa na hiyo tunaamini itapunguza sana migongano kati ya serikali na sekta binafsi”alisema

Alisema kuwa  wafanuabiashara wanajiona kama wameachwa na serikali na wala haitaki kuwahudumia na kwamba wanaonana na serikali wakati wa kodi na michango mbali mbali pekee.

0 comments: