Pages

Thursday, February 6, 2014

TAKUKURU yawafikisha mahakamani watumishi wanne wa halmashauri ya mbarali

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Mkoa wa Mbeya imewafikisha katika mahakama ya hakimu mkazi  Wilaya ya Mbarali  watendaji  wanne wa halmashauri ya Wilaya  hiyo kwa makosa  tisa likiwemo la kutoa malipo hewa  kwa  Watumishi.
 
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya  Gwaya Sumaye aliwataja washitakiwa hao kuwa ni pamoja na aliyekuwa mganga mkuu wa Wilaya ya Mbarali Dk Somoka Mwakapala ambaye amehamishiwa Wilaya ya  Handeni Mkoani Tanga.


Wengine  ni Francis Kapinga ambaye alikuwa mhasibu  wa idara ya  afya  katika halmashauri hiyo ambaye  kwa sasa amehamishiwa Morogoro vijijini  na Lazaro Mgimba mhasibu msaidizi wa halmashauri ya Wilaya ya Mbarali .

Akisoma mashitaka hayo Mwendesha mashitaka huyo aliyataja mashitaka yanyowakabili washitakiwa kuwa ni pampoja  mashitaka manne ya matumizi mabaya ya nyalaka  za serikali na mawili yakiwa  ya matumizi mabaya ya madaraka.

Aliyataja mashitaka mengine kuwa  kugushi nyalaka za serikali,uhujumu uchumi  na kuisababishia hasara Serikali  Sh3.4 milioni na kwamba katika makosa hayo washitakiwa  wanadaiwa kutoa malipo hewa kwa watumishi  hewa.

Alisema kuwa  washitakiwa walionyesha kuwa wametoa malipo ambayo ni hewa kwa watumishi  waliohudhulia mafunzo ya  magonjwa  yasiyopewa  kipaumbele kinyume na cha sheria na taratibu za malipo ya fedha za serikali.

Washitakiwa wote walikana mashitaka hayo  wako nje kwa dhamana na  kesi itakauwa Februali  20,2014 kwa ajili ya kusikiliwa.
 

0 comments: