Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza katika uzinduzi wa Rift ya kwanza Mkoani Mbeya katika jengo la Ghorofa sita mali ya chama cha Walimu Mkoa wa Mbeya
Walimu wakicheza kwa furaha katika uzinduzi wa Rift hiyo
Katibu wa chama cha Walimu Mkoa wa Mbeya (CWT) Kasuku Bilago akitoa taarifa ya Mkoa
Walimu wakiimba kwaya katika siku hiyo ya uzinduzi wa Rift
Katibu Mkuu wa CWT Yahya Msulwa akitoa hotuba katika uzinduzi huo
Mgeni rasmi Kaimu katibu tawala Mkoa wa Mbeya Nyasebwa akitoa hotuba kwenye uzinduzi huo
Katibu
Mkuu wa chama cha Walimu Tanzania (CWT) Yahya
Msulwa amesema kuwa chama hicho kinatarajia kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya
kuwasaidia Walimu katika kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.
Alitoa kauli
hiyo jana mara baada ya uzinduzi wa Rift ya kwanza Katika mkoa wa Mbeya kwenye jengo
jipya la chama hicho lenye ghorofa Sita lililojengwa
eneo la Soka matola jijini hapa na kuwa
ni jengo pekee refu katika jiji la Mbeya.
Alisema
kuwa mradi huo wa majengo ambao utajengwa
katika mikoa yote hapa nchini utawasaidia Walimu kama dhamana na kuweza kupata
fedha nyingi zinakazowekwa kwenye mfuko maalum utakoundwa kwa ajili ya
kuboresha maisha ya Walimu.
“Haya ni
majengo ya walimu wote ambapo mwalimu mmoja mmoja atanufaika na majengo haya
ambapo tayari mkakati umeandaliwa wa kuunda mfuko maalum ambao utakuwa unatoa fedha
kwa ajili ya kuwasaidia katika kuboresha maisha yao’alisema
Alisema
kuwa kuhusu aunzishwaji wa benki ya
Walimu tayari kiasi cha Sh 16 bilioni kimepatikana kwa ajili ya uwanzishwaji wa
benki hiyo na kwamba baada ya miezi miwili kuanzia sasa inaweza kuanza kufanya
kazi.
Msulwa
alisema kuwa benki hiyo itakuwa ya biashara ambapo walimu na watu wengine
watapata nafasi ya kupata mkopo na kwamba faida itakayopatikana benki itatoa
gawio na kurudi kwenye mfuko huo maalum wa kuwasaidia Walimu.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa CWT Mko wa Mbeya Mwl Nelusigwe
Kajuni alisema kuwa lengo la kuweka rift katika jengo
hilo ni kuwasaidia walimu wenye ulemavu kufika kwa urahisi katika ofis husika
na kuwez a kupata huduma wanazozihitaji.
Mwl Kajuni alisema kuwa malengo mengine ni kuongeza
tija na ufanisi wa kazi kwa watendaji wa
CWT na kwa jamii nzima inayowazunguka na kuhakikisha huduma zinatolewa kwa
wakati.
0 comments:
Post a Comment