Wadau wa Wakala wa vipimo Mkoa wa Mbeya wakiendelea na mkutano katika ukumbi wa Goden City Hotel
Kaimu katibu tawala Mkoa wa Mbeya (RAS)Leonard Magacha akitoa hotuiba yake katika mkutano wa wadau wa wakala wa vipimo Mkoa wa Mbeya.
Mbeya.Wakala wa
vipimo (WMA)ametakiwa kujiimarisha kwakufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo ya masoko ili
kuweza kutatua tatizo la Lumbesa linalosababisha wananchi na wakulima kudhurumiwa mazao
yao.
Kauli hiyo
imetolewa na Kaimu katibu tawala Mkoa wa
Mbeya Leonard Magacha katika mkutano wa
pamoja wa wadau wa wakala wa vipimo
uliofanyika katika ukumbi Mbeya Gorden City jijini hapa.
Magacha alisema kuwa suala la Lumbesa bado ni tatizo kubwa
linalowasumbua wakulima ambapo wachuuzi
wamekuwa wakijinufaisha kupitia lumbesa na kuwaacha Wakulima kuendelea kuwa masikini
kutokana na kushindwa kupata faida ya mazao yao.
“Tunahitaji
kuwa na ukaguzi wa kushitukiza wa mara kwa mara katika maeneo ya masoko yetu
ili tuweze kumaliza tatizo hili ,shirikianeni na serikali za vijiji na kata
pamoja na maafisa biashara wa Wilaya kwani peke yenu hamuwezi kufanikiwa katika
kuondoa kero hii”alisema
Alisema kuwa
mkoa wa Mbeya ni mkubwa na utaratibu unaotumika katika biashara ya bidhaa siyo
vipimo halisi kwani uchunguzi unaonyesha ni asilimia moja ya Mkoa mzima ndiyo wanatumia vipimo halisi.
Awali akitoa
taarifa kaimu meneja wa Wakala wa vipimo Mkoa wa Mbeya Deogratias Hussein alisema
kuwa wanakabilina na changaoto kubwa ya sheria kupita na wakati ambao adhabu
zinazotolewa kwa mkiukwaji wa vipimo ni ndogo na hivyo kushindwa kumaliza tatizo
la utumiaji wa vipimo visivyo halali hasa lumbesa.
Alisema kuwa
Katika sheria ya vipimo sura 340 iliyofanyiwa marekebisho 2002 inaeleza kuwa
atakaye patikana na hatia kutokana na
kutumia vipimo visivyo halali adhabu yake ni faini ya Sh10,000 kwa kosa la kwanza akirudia kosa basi atapewa
adhabu ya kulipa faini isiyo zidi Sh20,000 au kifungo cha miaka isiyodizi mitatu
jela.
0 comments:
Post a Comment