WIMBI la
Wizi wa mita za maji umeshamili jijini Mbeya ambapo ndani ya miezi miwili
kuanzia Juni hadi Julai zaidi ya mita 50
zimeibiwa.imeeelezwa
Kutokana na
kuwepo kwa tatizo hilo mamlaka ya maji safi na taka jiji la Mbeya(MUWASA)imetanganza
bingo kwa mtu yeyote ambaye atatoa taarifa sahihi ya mahali ambapo mita hizo zinapelekwa
atapewa fedha tasilimu Sh300,000.
Akizungumza
na gazeti hili Mwanasheria wa mamlaka hiyo Simon Bukuku alisema kuwa wizi wa mita hizo ulikuwa
ukitokea katika kipindi cha nyuma
kwa kiasi kidogo, lakini uliibuka
kwa kasi kubwa mwaka 2012.
“Wimbi kubwa
la wizi huu wa mita ulianza Julai 2012 hadi juni 2013 ambapo mita 256 ziliibiwa
ndipo tulipoanza kuchukua hatua mbali
mbali ikiwa ni pamoja na kufanya
uchunguzi na kutoa taarifa katika jeshi la polisi”alisema
```
Bukuku alisema kuwa baada ya uchunguzi kufanyika
walipata taarifa kuwa mita hizo zinapelekwa nchi jirani ya Malawi na kwenye
vituo vya kuuzia vyuma chakavu ambapo oparesheni ilifanyika lakini hawakuweza
kufanikiwa kuzipata mita hizo.
“Tulifanikiwa
hadi kufika nchini Malawi katika miji ya
Kalonga,Mzuzu na Lilongwe lakini hatukuweza kufanikiwa kuzikuta kwani wenyeji
walituambia kuwa hawakuwahi kuziona mita za Tanzania kwani hata wao wanaibiwa
mita hizo na idaiwa kuwa zinaletwa hapa kwetu Tanzania”alisema
Alisema
kutokana na uchunguzi huo wizi huo ulipungua kwani kulikuwa hakuna
matukio,lakini cha kushangaza ni kuibuka
upya kwa wimbi la wizi wa mita hizo kwa kutumia mbinu ya kunyofoa sehemu
ya katikati ya shaba ya mita hizo na
kuacha chuma cha nje.
“Kwa mwaka
huu hali imekuwa mbaya zaidi kwani ndani ya miezi miwili ya Juni na Julai 2014 jumla ya mita 54 zimeibiwa na kuanzia
February hadi Mei mwaka huu mita 69
hivyo vitendo hivi vimekithiri katika jiji letu”alisema
Alisema kuwa
maeneo ambayo ndiyo yamekithiri kuibiwa mita hizo ni pamoja na kata ya
Mwakibete,Ilomba na Luanda ambapo hatua mbali mbali zimeanza kuchukuliwa ikiwa
ni pamoja na kuwahamasisha wananchi kuhamisha mita zao kutoka nje ya wigo na kuzifunga ndani ili kuepusha
matukio ya wizi huo.
“Wakati
uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini mita zinapelekwa wapi na zinafanyiwa
nini, tunaomba ushirikiano wa karibu na wananchi kwani mita hizi zinaibiwa
kuanzia majira ya saa 11:00 hadi 12:45 alfajiri”alisema
Aidha
alisema kuwa hatua zingine zilizochukuliwa na mamlaka hiyo ni pamoja
kuziandikia barua za nchi jirani cha
Malawi na Zambia kuomba ushirikiano wa kuzibaini mita hizo na kupeana taarifa
endapo watazikamata mita hizo.
0 comments:
Post a Comment