Ustadhi Ibrahimu Mkate akizungumza katika Ibada ya Swala ya Idd El Fitri kwenye Viwanja vya Kiwanja Ngoma Sokomatola Jijini Mbeya jana asubuhi. |
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa katika Ibada ya Swala ya Idd jana asubuhi. |
Waumini katika Ibada ya Swala ya Idd el Fitri Jijini Mbeya jana asubuhi. |
JUMUIYA
ya waislamu wa Answar Sunna mkoani Mbeya wamesema kitendo cha mauaji na
utekaji nyara kinachofanywa na makundi ya Boko Haram na Alqaida ni uovu
unaopaswa kupingwa na waislamu kote duniani kwa kuwa si mafundisho ya
dini hiyo.
Akizungumza
wakati wa ibada ya kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani jijini
Mbeya Kiongozi wa Kiislamu ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha
Kiislamu cha King Saud kilichopo Riyadhi nchini Saudi Arabia, Ustadh Ibrahimu Mkate alisema watu hao wanapaswa kuuawa kutokana na kupingana na mafundisho ya Uislamu.
Alisema
kinachofanywa na watu hao kinapingana na dini ya Kiislamu hivyo
waislamu wanapaswa kuungana kupinga vitendo hivyo ili kuunusuru Uislamu
na waislamu duniani.
‘’Hii
si mila ya dini ya Kiislamu inayohubiri amani na upendo, hawa wanaowaua
watu wasio na hatia, mafundisho haya wanayatoa wapi,wanavaa mabomu na
kujilipua na kuwaua watu wasio na hatia, akina mama, wazee na watoto,
wao ndio wanaopaswa kuuliwa,’’alisema Ustadh Mkate.
Aliwakana
watu hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakijivika jina la Kiislamu na
kufanya mambo yanayoshabihiana na dini ya kiislamu kwa kuwaita kuwa ni
makafiri ambao wanaupinga Uislamu.
‘’Hawa ni maadui wa Uislamu, uislamu unafundisha Amani na Upendo, wanatuchafua waislamu, sisi hatufundishi kuuana bila hatia, zipo sheria zinazotanabahisha nani wa kuuliwa kwa wakati gani na kwa sababu gani,
Aliendelea kusema kuwa makundi ya Alshabab, Boko haram, Alqaida ni
makundi yasiyofaa katika Uislamu na kwamba kitendo chao cha kuvaa
mabomu na kujilipua ni ukafiri ambao hauendani na mafundisho ya Uislamu.
Alisema
kuwa hiyo si Jihadi kama inavyotafsiriwa bali ni ukatili na unyama
unaofanywa na maadui wa Uislamu ili kuuchafua na kuwa mafundisho ya
Muhammad (SAW) kwa waislamu yalikuwa ni kuingia vitani kupigania dini
yao kwa haki dhidi ya wale wanaowapinga na kuwaua bila haki na sio kuua
wasiokuwa na hatia.
‘’Hakuna
Sheria ya kujilipua mabomu kwa waislamu, hiyo sio Jihadi iliyosemwa,
huo ni Ukafiri na wanaofanya hivyo ni Makafiri sio waislamu,’’ alisema.
Kwahisani ya
0 comments:
Post a Comment