Mbeya.Vilio
na Simanzi vimetawala katika mji mdogo wa Mbaralizi Wilaya ya Mbeya vijijini baada ya Watu 10 kufa papo hapo akiwemo mama na mtoto wake, na wengine
nane kujeruhiwa baada ya Toyota Hiace walioyokuwa kisafilia
kugongana na roli katika eneo lilokaribu na kituo cha Mafuta.
Ajali hiyo
imetokea majira ya saa 6:00 mchana imehusisha gari aiana ya Toyota Hiace ailiyokuwa ikitokea Mwanjelwa kuelekea
Mbalizi na kuigonga roli aiana ya fuso lililokuwa
litokea katika kituo cha mafuta na kuingia barabara kuu ya kutoka Mbeya kwenda
Tunduma.
Akizungumza
katika hospitali teule ya Wilaya ya
Mbeya muuguzi mkuu wa hospitali hiyo
Sikitu Mbilinyi alisema kuwa katika hospitali hiyo wamepokea maiti 10 wakiwemo wanawake wanne,wanaume nne na watoto wawili.
Alisema kuwa
katika majeruhi nane,watano ni wanaume
na watutu ni wanawake na kwamba madaktari baada ya kubaini hali za majeruhi hao
kuwa mbaya walishauri wapelekwe katika hospitali ya rufaa Mbeya ambapo tayari
majeruhi watatu akiwemo mwanamke mmoa wamehamishiwa katika hospitali hiyo.
Aliwataja
waliokufa katika ajali hiyo ambao wametambuliwa na ndugu zao kuwa ni pamoja na Mariam
Mashambwe na mtoto wake Hamis Chaula,Rebeca Keneth,Petro mgogo,Haruna Jamison
na Martin Mwasolikoto.
Mbilinyi
aliwataja waliojeruhiwa na ambao wamelazwa
hospiotalini hapo kuwa ni pamoja
na Kondakta wa Hiace,Justin Chaula(28)mkazi wa mabatini,Kondakta
wa roli Joseph Stephano (22) mkazi wa
mbalizi , aliyekuwa abiria wa roli Ziona Goa (20),Newton Patrick na dereva wa roli Amoni Mwakoko.
Akizungumzia
jail hiyo majeruhi Ziona Goa alisema kuwa Hiace waliyokuwa wamepanda ilikuwa
inatatizo la Breki ambayo ilisababisha gari hilo kuwa na mwendo kasi huku mbele kukiwa na roli ambalo tayari
limeshaingia barabarani.
“Dereva wa
gari letu alisikika akisema kuwa breki hazifanyi kazi huku gari yetu ikiwa na
mwendo kasi na ghafla tunaona tayari mbele yetu kuna roli limeingia barabarani
na ndipo tulipoligonga ubavuni mwa roli hilo”alisema
Kamanda wa
polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amethimitisha kutokea kwa ajli hiyo na kwamba
uchunguzi wa ajali hiyo unafanyika ili kuweza kubaini chanzo cha ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment